Wednesday, 6 April 2011

U TRACK YAFUNGA VIFAA VYA KUDHIBITI MWENDO KASI KWENYE MABASI KWA MAKAMPUNI 11 NCHINI

Albert Kikala Meneja wa mradi wa kampuni ya Utrack akiwaelezea waandishi wa habari leo wakati alipozungumzia mpango wa kampuni hiyo, katika kupunguza ajali za barabarani kwa mabasi ya abiria kwa kufunga vifaa maalum ambavyo vinatuma taarifa za mwenendo wa dereva anayeendesha gari hilo. 
Akizungumzia kuhusu mradi huo amesema wanatumia gharama zao kwa ajili ya kunusuru maisha ya watanzania, ili kupunguza ajali za mabasi barabarani, ameongeza kuwa yeye ameshatembelea kampuni zaidi ya 130 na kuelezea mfumo huo na faida zake kwa wamiliki wa mabasi hayo, ambapo kwa sasa ni kampuni 11 zimeshafunga kifaa hicho. 


Amesema gharama za kufunga kifaa hicho kwa gari moja ni dola za kimarekani 472 zaidi ya shilingi za kitanzania 800.000, na kila mwezi kutakuwa na gharama fulani ambayo mmiliki wa gari atalipa dola 47 kwa mwezi ili kuendesha huduma hiyo Mitambo hiyo kwa sasa imefungwa katika makao makuu ya kampuni ya Utrack pale Namanga Mbuyuni jijini Dar es salaam, 

Makao makuu ya kikosi cha usalama barabarani na makao makuu ya Polisi ili kuleta ushirikiano katika kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua kama siyo kumalizika kabisa. Kifaa hicho kina uwezo wa kutuma taarifa za dereva jinsi anavyoendesha gari barabarani, kasi yake, kinauwezo wa kupiga picha kila kinachofanyika kwenye gari nataarifa zake zikatumwa makao makuu ya Utrack, Traffic na Makao makuu ya Polisi , katika picha kushoto ni Baraka Mohamed Mratibu wa Mradi

No comments:

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI