Tuesday, 24 December 2013

VIJANA WENGI WAMEKIMBILIA MJINI NA KUWAACHA WAZEE VIJIJINI WAKITESEKA,


     Katika ziara ya Mh. Vicky Kamata mkoani Geita alikutana na mambo mengi sana lakini familia hii ilikua ni kivutio cha kusikitisha kidogo, Vikongwe wawili walikuwa wakiishi pamoja maisha ya kujitegemea na walikua ki mtu na mkwewe, wakiishi maisha yaliyojaa kila aina ya dhiki ikiwemo kupata chakula kwa kuombaomba na kuishi nyumba duni huku wakionekana kuchoka kiasi cha kutomudu kufanya kazi yoyote inayoweza kuwaingizia kipato.
     Mara baada ya kufika kijiji na cha Nungwe Mh. Vicky alikutana na familia hii na ilikua na maisha ya kushangaza na yanayotia simanzi sana. ishuhudie katika picha.

Mmoja wa wazee ha akitoka kwenye nyumba wanayoishi yeye na mama wa mume wake [mkwewe]

Vikongwe hao wakiwa pamoja kulia ni Mama wa Mume wa Bibi wa upande wa kulia
Mh. Vicky akiongea kwa na Vikongwe hao na baadhi ya majirani pia walifika eneo la tukio

Mh.Vicky hakupenda wabaki hivihivi aliwazawadia kaga na pesa kidogo ya kujikimu.

Zawadi ya Kanga


katika picha ya pamoja na vikongwe hao

Wamependeza na zawadi zao za sikuuu hizi za mwisho wa mwaka.

Mh. Vicky akijaribu kuwauliza maswali
Nyumba wanayoishi

wakiwa na furaha baada ya kupata zawadi kutoka kwa Mh. Vicky

Hiki ni Choo na Bafu cha vikongwe hao

 

2 comments:

Anonymous said...

Inasikitisha hasa hizi nchi za bara hili la Africa, kama lilivyoitwa zamani dack continent, wazee kama hawa walikuwa wanaitaji msaada wa kusaidiwa na serikali na viongozi ndio kama hao wanakwenda na kuwapa tuzawadi tudogo tudogo na kuendelea kuwacha wakiteseka na maisha.

Anonymous said...

Alafu huku viongozi walio wengi wanaendelea kuishi maisha ya kifahari na anasa kwa kuribia Taifa mali za umma na kodi za wanachi, walio wengi ni masikini wa kutupwa

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI