Tuesday, 24 December 2013

WATOTO WANAOLELEWA NA VICTORIA FOUNDATION WALIPOPATA FURSA YA KUJUMUIKA NA FAMILIA ZAO GEITA. [PAGE 2]

Na Steven Mruma 

   Watoto wawili wanaolelewa na Victoria foundation Ernest Masuuko Sunguye na Jeremia Julius walipata fursa ya kuwa pamoja na familia zao kwa muda huu wa likizo, watoto hao wanaosomeshwa na kupatiwa matibabu pamoja na huduma zote za msingi na mfuko Victoria Foundation wanasoma shule iitwayo Salvation Army English Medium iliyopo jijini Dar es salam.
   Watoto hao mmoja ambaye ni Ernest anaishi Genge Saba na Jeremia Anaishi Nungwe mkoani Geita.

   Baada ya siku ya kwanza jioni Jeremia kuwasili kijijini kwao Nungwe siku iliyofuata Ernest Masuuko naye aliwasili kijijini kwao Genge saba na mambo yalikuwa kama picha zinavyoonyesha.

 
Njia inayoelekea nyumbani kwao Ernest

Mjumbe akienda kumpasha habari mama wa Ernest kua kuna ugeni unafika nyumbani hapo

Mama yake Ernest akisubiri kwa hamu ugeni wa mwanae na Mh. Vicky Kamata

Ernest akishuka kutoka kwenye gari
Karibu tena Nyumbani Ernest
Ernest akipokewa na Mama yake kwa furaha.

Hapa akisalimiana na mama yake
Mama Ernest akipokea wageni wengine walioambatana na Mh. Vicky

Dada Jesca ambaye ni katibu wa Mh. Vicky akiwa na Mgodo wake Ernest nayeitwa kalebo na kulia ni Mh. Vicky Kamata


Mh. Vicky Kamata [kushoto] Ernest [katikakti] na Mama Ernest[kulia]

Ernest akisalimiana na marafiki zake

Akibadilishana mawzo na watoto wenzake
Mh. Vicky akiongea na ndugu jamaa na majirani waliofika nyumbani kwao Ernest

Mh. Vicky Kamata akitoa wito kwa baadhi ya wanakijiji waliofika nyumbani kwao Ernest

Hapa Mh. Vicky akimzungumzia Ernest na Maendeleo yake ya shule

Mara baada ya muda kupita Baba yake Ernest Bwana Masuuko Sunguye aliwasili kumuona mwanaye na hapa akisalimiana na Mh. Vicky kamata

Baba wa Ernest akiwa na mwana mdogo na Mh. Vicky Kamata

Wengi waliofika nyumbani hapa hawakuondoka mikono mitupu, walipata zawadi ya Christmass na mwaka mpya kutoka kwa Mh. Vicky

Zawadi zikitolewa

Hata watoto pia hawakutoka mikono mitupu wote walipata hela ya sikukuu

Akina mama wakifurahia zawadi za kanga kutoka kwa Mh. Vicky Kamata

Mh. Vicky Kamata akiwa katika picha ya pamoja na akina mama na watoto waliofika nyumbani kwao Ernest, akina mama hao walikua wamevaa kanga walizopewa na Mh. Vicky.

No comments:

GEITA DOCUMENTARY