Monday, 23 December 2013

WATOTO WANAOLELEWA NA VICTORIA FOUNDATION WALIPOPATA FURSA YA KUJUMUIKA NA FAMILIA ZAO GEITA. [PAGE 1]

   Na Steven Mruma 

   Watoto wawili wanaolelewa na Victoria foundation Ernest Masuuko Sunguye na Jeremia Julius walipata fursa ya kuwa pamoja na familia zao kwa muda huu wa likizo, watoto hao wanaosomeshwa na kupatiwa matibabu pamoja na huduma zote za msingi na mfuko Victoria Foundation wanasoma shule iitwayo Salvation Army English Medium iliyopo jijini Dar es salam.
   Watoto hao mmoja ambaye ni Ernest anaishi Genge Saba na Jeremia Anaishi Nungwe mkoani Geita.

   Wa kwanza kufika kijijini alikuwa ni Jeremia na hali halisi ilikuwa hiuvi mara tu baada ya kuwasili kijijini.

Jeremia Julius

Jeremia akishuka kwenye Gari alipowasili kijijini kwao, Nungwe mkoani Geita

Akishuka kwenye Gari
Mama yake Jeremia akiwa haamini kumuona tena mwanaye Jeremia

Mama Jeremia akisalimiana na mwanaye
Mama Jeremia akisalimiana na Mh. Vicky Kamata na hapa alikua akimuonyesha jeraha alilolipata mguuni.

Mara tu baada ya kuwasili ndugu jamaa na marafiki walianza kukusanyika nyumbani kwa akina Jeremia

Ndugu jamaa na marafiki wakiwa nyumbani kumsalimia Jeremia
Mh. Vicky akiwa na furaha baada ya kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wanakijiji wa Nungwe

Jeremia alishindwa kujizuia na hapa alijikuta akilia kwa furaha baada ya kukutana na Ndugu jamaa na marafiki zake.

Baada ya salam Mama Jeremia aliingia jikoni kumuandalia Jeremia na wageni chakula.

Jeremia akiwa na rafiki yake Ernest na Kulia ni Mama Jeremia

Wengi walifika nyumbani kumuona Jeremia ambaye aliondoka akiwa mgonjwa.

Mh. Vicky Kamata akibadilishana mawazo na baadhi ya wanakijiji.
Mh. Vicky akiagana na wakijiji

Baadhi ya wanakijiji wakimsindikiza Mh. Vicky kwenye Gari

Mh. Vicky akiwaaga wanakijiji wa Nungwe.


No comments:

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI