Thursday, 26 December 2013

WALEMAVU NA WAJANE KUFADHILIWA VYEREHANI ZAID YA 100 NA VICTORIA FOUNDATION KUPUNGUZA UGUMU WA MAISHA

Na Steven Mruma [Geita]

     Walemavu na wajane watanufaika na ufadhili utakaotolewa na Victoria Foundation Kupitia kwa M/kiti wake Mh. Vicky Kamata ambaye ni mbunge wa viti maalum Geita, katika kuwezesha makundi hayo Victoria Foundation Itafadhili Vyerehani Zaidi ya Mia Moja (100+) vya kisasa kutoka Ujerumani na Uholanzi, na si hivyo tu pia Victoria Foundation itafadhili mafunzo ya walemavu hao na jinsi ya kutimia na kufanya matengenezo ya Vyerehani watakavyopatiwa.
    Mafunzo hayo yanataraji kuanza mapema mwakani maeneo ya Nyakato SIDO Mwanza katika Ofisi za SIDO mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya vyerehani vitakavyotolewa kwa walemavu na wajane
    Katika ufadhili huo pia baadhi ya walemavu watapatiwa Tool Box ambazo zitakuwa na vifaa mbalimbali vya ufundi wa Baiskeli na pikipiki ili kuweza kuwasaidia walemavu katika vikundi vyao kujikwamua na ugumu wa maisha,,

    Ufadhili huo pia unalenga kuwapa mitaji wajasiriamali walemavu na wajane ili waweze kuinua bishara zao na kazi zao mbalimbali za kiuchumi ili kuhakikisha wanapunguza ugumu wa maisha.  akizungumza na Viongozi wa Vikundi vya walemavu na wajane waliofika katika hafla fupi ya kutambua na kutafakari jinsi ya kuwapunguzia wajane na walemavu ugumu wa maisha, ambapo mgeni rasmi alikua Mh. Vicky Kamata ambaye aliahidi kupitia Foundation Ya Victoria Foundation Kusaidia na kufadhili miradi hiyo ili kuwawezesha walemavu, watoto yatima, watoto wa mitaani, wajane na walemavu.
   Aidha Mh. Vicky alisema imani yake kubwa mlemavu pekee anayeweza kusimama kama mleamavu ni mlemavu wa akili tu lakini hawa wengine si walemavu na kwamba hilo ni jina tu lakini wanaweza kuyatengeneza maisha yao zaidi ya binadamu wengine waliokamilika viungo vyote.
    Aliongeza pia wanachokosa sana ni kuwezeshana tu na nafasi waliyoipata kutoka Victoria Foundation waitumie kikamilifu na pia ikawe elimu kwa wenzao sehemu mbalimbali kuwa hata walemavu pia wanaweza hasa wakiwezeshwa.


Mh. Vicky Kamata akizungumza na Viongozi wa vikundi mbalimbali vya walemavu na wajane


Picha ya pamoja na viongozi wa vikundi vya walemavu,

Picha ya pamoja na viongozi wa vikundi vya walemavu


 
Mh. Vicky akijiandaa kupiga picha na Viongozi wa vikundi vya wajane.
Picha na Viongozi wa Vikundi vya wajane Geita


Mh. Vicky Akipeana mikono na viongozi wa vikundi vya wajane.


No comments:

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI