Wednesday 26 May 2010

Ray C: Mwanamuziki anayeikumbuka kazi yake ya zamani


UVUMILIVU ni kitu cha msingi sana katika maisha ya mwanadamu kila siku hasa inapotokea unataka kufanya kitu fulani ambacho baadae kinaweza kikakuletea manufaa ambayo ulikuwa umeyasubiri kwa muda mrefu.

"Kwa mfano wakati naanza fani hii ya kuimba, watu wengi sana waliongea, wengine waliniambia hujui kuimba, wengine watakuambia hili na lile ilimradi tu kunikatisha tamaa katika fani ambayo ndio kwanza nilikuwa naingia," anasema Ray C.

Uvumiliivu pia unakwenda sambamba na muenekano na usikivu, kama msanii ni lazima uwe na 'good personality' kwa watu wote ili uweze kuuza kazi zako na uweze kukubalika kwenye jamii, pia wasikilize mashabiki wako, wakubwa zako, DJs na wadau mbalimbali wa fani ya muziki," anasema Ray C.

Ushauri huo umetolewa na msanii nguli katika miondoko ya Bongo fleva nchini ambaye inasemekana ndiye msanii wa kike mwenye mvuto kushinda wote Afrika Mashariki, Rehema Chalamila, wapenzi wa muziki wake wanamtambua zaidi kwa jina Ray C.

Ray C mwenye umri wa mika 28 hivi sasa, jina lake lilianza kuvuma alipokuwa mtangazaji redioni kabla hajaamua kuingia rasmi kwenye ulimwengu wa muziki, sio tena kama DJ bali muimbaji na mwanamuziki.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni Ray C anasema safari yake ya muziki ilianzia toka alipokuwa mdogo kwa kupenda kuwasikiliza wanamuziki mbalimbali wa enzi hizo kama Bi. Shakira (mwimbaji wa taarabu) na Remmy Ongala.

"Lakini pia nilikuwa napenda sana kusikiliza nyimbo za kihindi na pia kuangalia sinema za kihindi, nilikuwa sio msikilizaji mzuri sana wa redio kipindi hicho, nakumbuka nilichokuwa nakifanya wakati nikiangalia sinema za kihindi ni kwamba wanapofikia tu sehemu ya kucheza unajua tena movie za kihindi, kila baada ya action fulani, muziki unafuata nachukua kalamu na karatasi naandika wanachoimba kwa kiswahili," anasema.

"Ilifikia mahali ikawa mtu akiniambia niimbe wimbo fulani wa kihindi nakuimba wote lakini bila hata kuelewa maana yake, ingawa sikujua wakati huo kumbe ndio taratibu nikawa najifunza uimbaji, nadhani ndio maana hata hivi leo ukisikiliza vizuri baadhi ya nyimbo zangu utasikia zina baadhi ya vionjo au mahadhi ya kihindi hivi," anasema.

Anasema katika kila kitu ambacho mwanadamu atakihitaji kukifanya kwa ajili ya maisha yake ya baadae lazima kitakuwa na mwanzao na hata kwa upande wangu kama sio watu fulani leo hii asingekuwa msanii na ingewezekana angeishia katika fani ya utangazaji tu kama ilivyo kwa wengine ambao alianza nao kazi ya kutangaza.

"Kuna watu wawili watatu ambao walinishawishi kuingia katika muziki lakini sana ni Ruge Mutahaba ambaye wakati huo ndiye aliyekuwa meneja wangu pale Clouds FM, nakumbuka mara nyingi kila baada ya kumaliza kufanya kipindi changu redioni alikuwa akinisikia nikiimbaimba kwenye 'corridors' za pale ofisini", anasema.

"Nakumbuka akanishauri kama ninapenda kuimba na ningependa kurekodi basi nifanye mazoezi zaidi ya uimbaji, nitafute mtu aniandikie wimbo au niandike mwenyewe niingie studio kurekodi japo single moja kwanza na kisha kama itakuwa nzuri basi yeye angenisaidia kurekodi albamu nzima," anasema.

2 comments:

Anonymous said...

I аm actuаlly gгateful to the holder of thiѕ site whο has shared thiѕ grеаt paгagraph at at thіѕ plаce.
My web-site :: work at home jobs

Anonymous said...

Thanks , I've just been looking for information approximately this
topic for ages and yours is the best I've found out so far.
However, what concerning the conclusion? Are you certain in regards to the source?


my weblog ... Web Fortune Vault Review

GEITA DOCUMENTARY

Contributors