Friday, 28 May 2010
Mayaula afariki
MWANAMUZIKI mkongwe wa Jumahuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Fredy Mayaula Mayoni, amefariki dunia jana jijini
Brussels, Ubeligiji, kwa ugonjwa wa kansa ya ubongo.
Marehemu Mayaula Mayoni (64) ni mwanamuziki aliyekulia na kusomea jijini Dar wakati wa utoto wake miaka ya 60.
Mayoni, baba yake alikuwa ni mmoja
wana diplomasia katika ubalozi wa Congo (Zaire) nchini Tanzania.
Pia, marehemu aliwahi kuicheza timu Yanga ya Dar es Salaam miaka ya nyuma.
Marehemu Mayaula, atakumbukwa zaidi alipojiunga na bendi ya TP OK Jazz, iliyokuwa ikiongozwa na gwiji la muziki, Franco Luambo Makiadi nchini DRC.
Mayaula alijiunga TP OK Jazz baada ya kurudi kwao na kujihusisha zaidi na muziki na kufanikiwa kurekodi wimbo wa Cherie Bondowe au Sherry bondowe, wimbo ambao ulimpa umaarufu sana.
Mbali na TP Ok, aliwahi kufanya kazi na mwanamuziki Mpongo Love ambate pia ni marehemu.
Mungu amlaze pema peponi Mayaula Mayoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Post a Comment