Monday 7 May 2012

MAWAZIRI KUAPISHWA JUMATATU LEO





THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUAPISHWA KWA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, atawaapisha Mawaziri na Naibu MawaziriJumatatu tarehe 7 April, 2012, saa 5 asubuhi katika viwanja vya Ikulu.

Kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli hii, Nawaomba wahariri mtutumie majina ya waandishi waandamizi ambao watafika ikulu mapema saa 4.00 asubuhi kwa ajili ya shughuli hii.

Tunaomba majina hayo ya wawakilishi wa vyombo vyenu yawasilishwe kwetu mara baada ya kupata taarifa hii na mwisho wakupokea majina itakuwa  saa 2.00 asubuhi ya Jumatatu, kwa sababu ifikapo saa 4.00 kamili asubuhi kila mwalika anatakiwa awe tayari ameshakaa kwenye sehemu yake aliyopangiwa.

Tunapenda kusisitiza kuwa waandishi watakaoruhusiwa kuhudhuria shughuli hii ni wale tu ambao tutapokea majina yao kutoka kwa wahariri wa vyombo husika. Aidha, tunasisitiza mavazi yawe nadhifu na heshima, kwa kuwa hii ni shughuli ya Kitaifa.


Tunaomba ushirikiano wenu na karibuni.

……..Mwisho…..

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors