Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya Ikulu asubuhi hii ili kuanza kazi ya kuapisha mawaziri wapya aliowateua hivi karibuni Fullshangweblog ikiwa katika viwanja vya Ikulu inashuhudia kuapishwa huku kwa mawaziri na kukuletea moja kwa moja kutoka viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kabla ya kuanza kwa kuapiswa mawaziri hao.
Dk. Harrison Mwakyembe akila kiapo kuwa waziri wa Uchukuzi mbele ya Rais Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Iku asubuhi hii.
Shamsi Vuai Nahodha akila kiapo kuwa waziri wa Ulinzi mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Dk Husein Mwinyi akila kiapo kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Profesa Jumanne Maghembe akisaini kiapo mara baada ya kuapa kuwa waziri wa maji na umwagiliaji
Hawa Ghasia akila kiapo
Mh. Mathias Chikawe waziri wa Sheria na Katiba.
Mh. George Mkuchika akipongezwa na Rasi mara Baada ya kula kiapo.
Kwa hisani ya fullshangweblog.com
No comments:
Post a Comment