Monday, 28 July 2014

BAADA YA KUKUTANA NA MH. VICKY KAMATA, WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU GEITA WALILIA KUPATA SEHEMU YA UHAKIKA YA KUCHIMBA MADINI GEITA

Na Steven Mruma [Geita]
      Hivi karibuni Mh. Vicky kamata mbunge wa viti maalum Geita akichangia hoja Bungeni aliiomba serikali isikilize kilio cha wachimbaji wadogo wa dhahabiu mkoani Geita kwani uchumi wa wachimbaji hao wadogo unategemea sana kazi ya uchimbaji wa Dhahabu.
     Baadha ya kutoa ombi hilo kwa serikali iwatengee eneo maalum lenye dhahabu ya kutosha, hakuishia hapo Mh. Vicky alikwenda na kukutana na wachimbaji wadogo wa dhahabu na kusikiliza zaidi kilio chao huku wengi wakilia ugumu wa maisha kutokana na kukosa sehemu ya uhakika ya kuchimba madini hayo, kilio cha wachimbaji hao wa madini kilifika mbali zaidi baada ya wachimbaji hao kutaka eneo la uhakika lenye uzalishaji baada ya kutakiwa kuhama eneo la Samina kupisha muwekezaji.
      Baada ya kusikiliza kilio hicho cha wachimbaji wadogo wa Samina Mh. Vicky kamata aliwasihi wachimbaji hao watulie na kwamba kilio chao hakijadharauliwa na serikali na kuwaahidi kuwa muda si mrefu serikali itatoa majibu baada ya mazungumzo kati ya GGM na serikali.


Mh. Vicky Kamata akibadilishana mawazo  na baadhi ya viongozi, 
Mh. Vicky Kamata akizungumza na wachimbaji wadogo wa Dhahabu Geita

Mh. Vicky Kamata akisisitiza jambo alipokutana na kuzungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu
      

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors