Saturday, 2 August 2014

PICHA: CHADEMA WATWANGANA KAVUKAVU GEITA BAADA YA KUTOKEA FUNUNU YA KUTUHUMIANA MAMBO YA "MLUNGULA"

Na Steven Mruma credit to  Victor Bariety via Malunde1 blog, Geita

       Katika tukio lisilo la kawaida baadhi ya Viongozi wa juu wa CHADEMA Geita walijikuta wakizichapa kavukavu baada ya kutuhumiana mambo ya rushwa nadani ya Chama hicho baada ya wenzao,wakiwemo viongozi wa matawi zaidi ya 50 kukamatwa na vijana wa ulinzi wa chama hicho (Red Brigade) wakiwa katika hoteli ya Wandela mjini Geita wakiwa kwenye kikao cha siri na kudaiwa walikuwa wanapokea rushwa kutoka kwa wagombea.
        Kundi hilo la siri linadaiwa kuandaliwa na katibu wa Jimbo la Geita aliyepo sasa hivi Rogers Ruhega ikiwa ni mkakati wa kumuwezesha kurudi madarakani katika uchaguzi unaokuja ambao inaonekana ameelemewa na mgombea mwenzake Mutta Robert.
       Ruhega ambaye hakuwepo katika kikao hicho, inadawa wajumbe waliokutwa Hotelini hapo ni kundi lina lohaha kila siku kutaka arudi madarakani kwa gharama yoyote na moja ya mbinu walizokuwa wanatumia ni kuchafua mgombea mwenzake na kutoa rushwa.

        Tukio hili linashangaza na linaashiria ni jinsi gani baadhi ya Viongozi walivyokua na uchu wa madaraka kiasi cha kutumia njia za mkato ili kuingia madarakani, na huku ni kukosa uzalendo na mfano wa viongozi hawa ni dhahiri wanataka kulinda maslahi yao bali si kutatua na kuwasadidia wanachi wa Geita, na Taita kwa ujumla.  

      KWA KUSOMA KISA HIKI KWA UNDANI BOFYA HAPA [ CLICK HERE]
  
Hapa likua ni mara baada ya Red Brigades wavamia hotel na kukuta wenzao wanajichana kwa soda na maji kabla ya timbwili
Wafuasi wa CHADEMA wakitaka kuzichapa nje ya Wandela hotel mjini Geita katika tukio la wanachama chama hicho kukutwa kwenye kikao cha siri katika hotel ya Wandela iliyopo Shilabela mjini Geita, ambapo kwenye kikao hicho ilidaiwa walikuwa wanagawiwa mlungula ili kupitisha kambi ya Katibu wa CHADEMA jimbo la Geita Rogers Luhega ambaye yuko taabani kisiasa dhidi ya mpinzani wake Mutta Robert aliyeomba kugombea nafasi hiyo.
Vurugu zikiendelea nje ya Hotel hiyo vijana wa CHADEMA wakitunishiana misuri
Timbwili la aina yake likiendelea.
Red Brigades wakiwa nje ya hotel wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini kabla ya kutoa sintofahamu ya kukunjana.

No comments:

GEITA DOCUMENTARY