Friday 31 August 2012

Wanawake Mbeya watahadharishwa na pedi feki


WANAWAKE mkoani Mbeya wanapaswa kujihadhari na bidhaa feki wanazotumia hasa za kujisitiri wakati wa siku zao (hedhi).
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima na kuthibitishwa na baadhi ya wanawake umebaini bidhaa hizo feki zimekuwa zikiwavimbisha wanawake pindi wanapozitumia.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema uwepo wa bidhaa zisizothibitishwa viwango vya ubora kwa kiasi kikubwa inachangiwa na kukosekana kwa ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Walibainisha kuwa hali hiyo imechangia bidhaa nyingi zinazoingia mkoani Mbeya kupitia mipaka ya Kasumulu kwa upande wa nchi ya Malawi na Tunduma kwa upande wa Tanzania kuwafikia walaji na watumiaji bila ya kukaguliwa ubora wake, hali ambayo ni hatari kwa afya zao.

Aidha, mmoja wa wamiliki wa viwanda vya kuzalisha mafuta ya alizeti kwenye soko la Sido eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya, Sophia Adamu, alisema hakuna ukaguzi wowote unaofanywa na TBS kwa mafuta yanayozalishwa kwenye viwanda vyao na kupelekwa moja kwa moja kwa walaji bila ya kuthibitishwa ubora wake na shirika hilo.
Alisema tangu ameanza kufanya biashara hiyo hajawahi kuwaona TBS wakienda kukagua bidhaa zao na kuthibitisa ubora na akashauri shirika hilo kufungua matawi mikoni hususan Mkoa wa Mbeya ambao una viwanda vingi vidogo vidogo.

Na freemedia.co.tz 

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors