WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, ameondoa hofu Watanzania juu ya mfumo mpya wa usahihishaji mitihani utakaoanza kutumiwa mwaka huu na kusema kuwa ni mzuri.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mpango kazi wa uwezeshaji wa wanawake na wasichana, alisema mfumo huo unalenga kurahisisha usahihishaji, na wanautumia kwa kuwa kuna tafiti maalumu zinafanywa kuhusiana na elimu.
“Mfumo huu tunautumia kwa kuzingatia kwa sasa kuna wanafunzi wanaofika milioni 8.3. Mfumo huu si mgeni kwani unatumiwa katika nchi za Pakistan na Marekani ambako kuna wanafunzi wengi, hivyo wananchi wasiwe na hofu kuhusu njia hii ya usahihishaji,” alisema.
Na freemedia.co.tz
No comments:
Post a Comment