Thursday, 12 April 2012

Mutharika kuzikwa April 23


IKULU ya Malawi imethibitisha jana kuwa mazishi ya Rais wake wa tatu, Bingu wa Mutharika yatafanyika Aprili 23, mwaka huu katika shamba lake lililopo Ndata, Wilaya ya Thyolo, kusini mwa Mji wa Blantyre.

Uamuzi huo unakwenda sambamba na ule wa kuongezwa kwa siku za maombolezo kutoka 10 hadi 30, ili kuyapa maombolezo hayo uzito unaolingana na msiba wa “mkuu wa nchi aliyefariki dunia akiwa madarakani.”


Awali, kabla ya Rais Banda kuapishwa, Ofisi ya Rais na Baraza la Mawaziri (OPC) ya Malawi, ilitoa taarifa kwamba kungekuwa na siku 10 tu za maombolezo ambazo zilitarajiwa kumalizika Jumapili wiki hii.

Lakini kutokana na kuongezeka kwa siku 20 zaidi, maombolezo hayo yanatarajiwa kukoma ifikapo Mei 6, mwaka huu na katika kipindi chote hicho, bendera zitaendelea kupepea nusu mlingoti huku televisheni na redio zikipiga muziki wa maombolezo.


Ofisa habari wa Ofisi ya Rais, Ruth Sandram alisema viongozi kadhaa wa Afrika akiwamo Rais Jakaya Kikwete wanatajia kushiriki katika mazishi hayo. Wengine ni Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Robert Mugabe wa Zimbabwe, Michael Satta wa Zambia na Armando Guebuza wa Msumbiji.

“Sasa ni rasmi kwamba hayati Mutharika atazikwa Aprili 23 na ni vigumu tarehe hiyo kubadilishwa kwa sababu tayari Rais (Banda) ameshawasiliana na viongozi wa nchi za Tanzania, Afrika Kusini, Zambia, Msumbiji na wengineo,”alisema Sandram.

Hata hivyo ofisa huyo alisema hana uhakika ni viongozi wangapi ambao wamethibitisha kushiriki mazishi hayo mpaka sasa lakini akasema vyombo vya habari vitaarifiwa wakati mwafaka.

Mwili wa Mutharika sasa unatarajiwa kuwasili Lilongwe Jumamosi badala ya leo ukitokea Pretoria, Afrika Kusini ambako kiongozi huyo alipelekwa kwa matibabu, lakini habari zinasema hakuwahi kupatiwa tiba huko kwani alikuwa tayari amefariki dunia.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Mutharika ambaye pia ni Waziri wa Serikali za Mitaa, Henry Mussa alisema jana kuwa: “Mwili wa marehemu sasa utawasili Jumamosi na kwamba mabadiliko hayo yanalenga kuipa Serikali muda zaidi wa majadiliano na familia ya marehemu.”

Juzi katika mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari tangu aapishwe kushika madaraka ya juu nchini Malawi, Rais Banda alisema alikutana na Waziri wake wa Mambo ya Nje, ambaye ni mdogo wa Marehemu, Peter Mutharika kujadili jinsi ya kuihitimisha safari ya kiongozi wao.

Mabadiliko katika mchakato wa mazishi ya Mutharika yanatokana na ukweli kwamba katika mipango ya awali, Banda wakati huo akiwa Makamu wa Rais hakushirikishwa lakini baada ya kuapishwa familia imejikuta haina njia ya kufanya mazishi bila idhini na baraka za Serikali.

Habari zinasema Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais na Baraza la Mawaziri, Bight Msaka aliiambia familia ya Mutharika na baadhi ya mawaziri waliokuwa wakifanya taratibu za awali za mazishi kwamba: “Wasingeweza kuratibu mazishi ya kiongozi mkuu wa nchi, nje ya utaratibu wa Serikali ambayo kwa mujibu wa Katiba kiongozi wake ni Makamu wa Rais baada ya Rais kufariki dunia.”

Maombolezo
Jana, Serikali liruhusu wananchi kwenda Ikulu ya Malawi (maarufu kwa jina la Nyumba ya Chifumu) kuhani msiba wa Mutharika na kuipa pole familia ya kiongozi huyo. Hatua hiyo inakwenda sambamba na kufunguliwa kwa makazi yake katika Shamba la Ndata, Blantyre atakakozikwa.

Kuwepo kwa sehemu rasmi za maombolezo huenda kukabadili sura za Miji ya Blantyre na Lilongwe ambako wananchi hawakuonekana kama wako katika maombolezo, huku alama ya pekee ya maombolezo hayo ikiwa ni bendera kupepea nusu mlingoti.

Katika Ikulu ya Lilongwe jana, watu wa marika tofauti wengi wakiwa ni wafuasi wa kilichokuwa chama tawala kabla ya kifo cha kiongozi huyo cha Democratic Progressive Party (DPP), walionekana wakiingia na kutoka baada ya kuwafariji wafiwa akiwamo mjane wa marehemu, Callista Mutharika.

DPP sasa ni chama cha upinzani baada ya kuapishwa kwa Banda ambaye tayari alikuwa amekosana na Mutharika hivyo kuamua kuanzisha chama chake kiitwacho Peoples Party (PP) akilenga kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika mwaka 2014.

Viongozi kadhaa wa DPP wakiwamo wabunge, wamekuwa wakiitisha mikutano na waandishi wa habari kutangaza kujiondoa katika chama chao na kujiunga na PP, hatua ambayo imekuwa ikitafsiriwa na wachunguzi wa mambo ya siasa kuwa ni  ‘unafiki wa kisiasa’.

Hata hivyo, juzi Rais Banda alisema wanasiasa hao hawapaswi kuwa na haraka ya kukimbia chama chao na kuwashauri wasubiri hadi Taifa lihitimishe maombolezo ya msiba wa Mutharika.

“Kuna wakati wa siasa unakuja, hebu sasa watulie wasubiri tumalize maombolezo ya kiongozi wetu. Hata hivyo, PP kina utaratibu wake wa kujiunga ambao lazima mtu aufuate na kukidhi matakwa ya masharti yaliyopo,”alisema Banda.
Aapisha Makamu wa Rais
Habari zilizopatikana jana jioni zinasema kuwa Rais Banda amemteua Naibu Katibu Mkuu kutoka chama chake cha PP, Khumbo Kachali kuwa Makamu wa Rais katika kipindi ambacho Malawi inatarajiwa kuwa na mabadiko makubwa ya kisiasa.

Kachali alithibitisha uteuzi wake alipozungumza na gazeti hili kwa simu huku akiahidi kuwa mtiifu kwa Rais Banda.

4 comments:

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

whoah this weblog is fаntastic i like readіng your posts.

Keep up the great woгk! You recognizе, many people are seаrching around for thiѕ info, you coulԁ helρ them greatly.


Mу homеpagе; submission software
My web site > Improve Google Ranking

Anonymous said...

Hey! This іs kind оf off topic but I need somе
aԁviсe frоm аn eѕtablіshed blog.
Is іt ѵегy hard to ѕet up
your oωn blog? I'm not very techincal but I can figure things out pretty quick. I'm thіnkіng abоut setting up mу οωn but Ι'm not sure where to start. Do you have any points or suggestions? Appreciate it

Here is my web blog; Improve Page Rank
Stop by my website : submission software

Anonymous said...

Hi, everуthing iѕ going nісеly hегe
аnd ofcoursе every onе is sharing facts, that's truly excellent, keep up writing.

Look into my blog ... Submit your website

GEITA DOCUMENTARY

Contributors