Wednesday 3 August 2011

MUBARAK KUJIBU MASHTAKA YA MAUAJI MISRI

Ulinzi mkali umedumishwa katika mji mkuu wa Misri, Cairo ambako aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak anatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Inaarifiwa kuwa maafisa wa usalama walifyatua risasi hewani katika bustani ya Tahrir Square ili kuwatawanya waandamanaji.

Mubarak ambaye aliondoka madarakani mwezi wa Februari anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi pamoja na mauaji ya mamia ya waandamanaji.
Mawakili wake wanasisitiza kuwa mteja wao ni mgonjwa sana na kuna idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo hawaamini ikiwa atafika mahakamani kujibu mashtaka dhidi yake.

Kwa raia wengi wa Misri Rais mubarak alikuwa sawa na mungu ambaye alitawala maisha yao kuwa muda wa miaka 30. Kwa kipindi chote hicho theluthi moja ya idadi yoye ya raia nchini humo hawajamjua kiongozi wowote ule.

Ahmed Shawky al Aqabawi mhadhiri wa somomo la sikologia katika chuo kikuu cha misri anasema watu wengi wanachuki naye na wamepania sana kuona amefungwa jela.
Wakuu wa jeshi ndio wanaotawala misri tangu Rais Mubarak aondelewwe madarakani.

Hata hivyo kwa siku za hivi karibuni uhusiano kati ya raia na viongozi wa kijeshi umekuwa mbaya. Wengi wanaamini kuwa utaratibu watakao chukua kuendesha kesi dhidi ya Hosni Mubaraka ndio utakaoamua uhusiano kati ya wakuu wa jeshi na raia utakuwa Hkatika siku za usoni.

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors