Tuesday 19 April 2011

WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA DAR

 Rais Jakaya Kikwete akiongea na Omary Nundu Waziri wa Uchukuzi kutoka Tanzania wa pili kutoka kulia, mara baada ya kuwasili katika katika hoteli ya Kempiski jijini Dar es salaam tayari kwa kupokea wageni wake, ambapo mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanyika kuanzia leo, wakuu hao watajadili mambo mbalimbali ya kimaendelea kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuchagua Katibu Mkuu mpya, atakayechukua nafasi ya Juma Mwapachu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo kutoka Tanzania, Katika picha katikati ni Balozi Chirau Ali Makwere Waziri wa biashara wa Jamhuri ya Kenya na kulia ni Dr. Shukuru Kawambwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Tanzania.

 Maofisa mbalimbali wakisubiri kuanza kwa mkutano kutoka kulia ni Asther Mkwizu Mwenyekiti wa Mfuko wa sekta binafsi Tanzania, Mh. Abdallah Mwinyi Mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania na mwisho ni Robert Bayigamba Mwenyekiti wa sekta binafsi nchini Rwanda.

Mawaziri wa Tanzania na Kenya wakijadili jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski leo asubuhi kutoka kulia ni Dr. Harrison Mwakyembe Naibu waziri wa Ujenzi, Dr Shukuru Kawambwa Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Omary Nundu Waziri wa Uchukuzi na Balozi Chirau Ali Makwere Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Kenya

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors