Tuesday, 19 April 2011

MAKAMU WA RAIS ATIA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS WA BRAZIL

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha rambirambi wakati alipofika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Brazil nchini, kuweka saini katika kitabu hicho maalum kutokana na kifo cha Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo,Jose Alencar da Silva, aliyefariki dunia hivi karibuni. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akizungumza na Balozi wa Brazil nchini, Francisco Soares Carlos Luz, wakati Makamu alipofika kwenye Ofisi za ubalozi huo Dar es Salaam, kwa ajili ya kutia saini katika kitabu cha rambirambi cha aliyekuwa Makamu wa rais wa zamani wa Brazil, Jose Alencar da Silva, aliyefariki hivi karibuni nchini humo. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais


No comments:

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI