Wednesday 14 August 2013

NECTA: MITIHANI KUSAHIHISHWA KWA COMPUTER, ITAONGEZA UBORA WA USAHIHISHWAJI.



Joyce Ndalichako

          Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Joyce Ndalichako amesema baraza lake linajiandaa kutumia teknolojia ya kompyuta wakati wa kusahihisha maswali ya mitihani ambayo wanafunzi wanajibu kwa kujieleza.
Kwa sasa teknolojia ya usahihishaji kwa kompyuta inayotumika nchini ni ile ya kujibu maswali ya kuchagua tu ya`Optical Mark Reader’ (OMR) iliyoanza kutumika mwaka jana kusahihisha mitihani ya darasa la saba.
     
Akizungumza na mwandishi wa habari jana wakati wa Mkutano wa Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA), unaoendelea mjini hapa, Dk Ndalichako alisema: “Kwa kuanzia, Necta itafanya majaribio ya teknolojia hiyo mwakani na ninaamini itaongeza ubora katika usahihishaji.”
“Kwa kutumia hii teknolojia msahihishaji hawezi kuona namba ya mwanafunzi, anachoona ni sehemu ya swali anayotakiwa kusahihisha na jibu lake, akimaliza swali moja jingine linakuja moja kwa moja,” aliongeza.
   Alisema kwa kutumia teknolojia hiyo, mratibu wa usahihishaji anaweza kuona kazi inayofanywa na msahihishaji yeyote na hata kuwapima kama atakuwa na wasiwasi wowote.
    Alisema Zimbabwe imeanza kutumia teknolojia hiyo aliyosema itasaidia kuongeza ubora katika suala la usahihishaji.
     Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jana, alisema teknolojia ya OMR imeongeza ubora wa hali ya juu kwenye mtihani wa darasa la saba pamoja na usahihishaji wake.
“ Watu wanasema kuwa mtihani wa maswali ya kuchagua ni mrahisi, lakini hii siyo kweli, inatungwa na wataalamu na inalenga kumpima mtoto katika kila nyanja, ndiyo maana hata mtihani wa darasa la saba mwaka jana ilibidi Serikali ishushe alama za kwenda kidato cha kwanza zikawa 70 badala ya 100,” alisema Dk Ndalichako.
        Akizungumzia teknolojia hiyo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema wamebaini kuwa zaidi ya asilimia 80 ya nchi za Afrika zinatumia mfumo wa usahihishaji kwa OMR.
    Alisema baadhi ya nchi zimeanza kusahihisha kwa kutumia kompyuta hata katika maswali ya kujieleza na kuwataka Watanzania kuacha kujirudisha nyuma.

1 comment:

Anonymous said...

Βut nоt only limіtеd for oгdinary occаѕiоns since it can easilу be used for special οccаsions as
well. It has an exquisite touch of fruіts and it lаsts lοng sо
you do not have to reapply it аll the time and this iѕ what
moѕt womеn look for in their perfume. Wоmen in the dating scenе arе embracing
the mаnу strаtegic aspectѕ of а peгfume thаt cοntains pherοmonеs.


Also visit my ωebρage; perfumes

GEITA DOCUMENTARY

Contributors