Wednesday 25 July 2012

PICHA ZA MATUKIO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA MNAZI MMOJA LEO !!!



Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam kuhudhuria sherehe za Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa.

Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwasili katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo kuhudhuria maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa. Hapo akisalimiana na wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana Vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyikia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Raisi Dkt. .Jakaya Mrisho Kikwete akiweka Ngao na Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Wa kwanza kutoka kushoto ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, Makanu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Raisi wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Raisi wa Zanzibar Balozi Seif Idd, Raisi Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai, Nahodha na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq, wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo kuhudhuria sherehe za Maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa Tanzania.




No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors