Wednesday, 25 April 2012
LEO NI SIKU YA MALARIA DUNIANI
Shirika la Afya Duniani, WHO, inaripoti kwamba mwaka 2009 takriban watu bilioni 3.3, ikiwa ni nusu ya wakazi wote duniani, walikabiliwa na hatari ya kuambukizwa na malaria. Kila mwaka hiyo inapelekea watu milioni 250 kuugua homa ya malaria na kusababisha karibu vifo elfu 850.
Mkutano mkuu wa wa 60 wa Shirika la Afya Duniani ulizindua rasmi siku ya malaria duniani mwaka 2007 kuadhimisha juhudi duniani za kudhibiti ugonjwa wa Malaria.
Siku hii ni ya kutathmini maendeleo yaliyopatikana katika kudhibiti na kutokomeza kabisa malaria, pamoja na kuhamasisha upya juhudi kuelekea lengo la kutokuwepo tena kifo hata moja kutokana na malaria ifikapo 2015.
Kundi la madaktari wasio na mipaka linasema Malaria ni muuaji mkubwa wa watoto chini ya umri wa miaka mitano katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. Kundi hilo la wataalamu wa afya linasema nchi zilizoendelea zinatakiwa kuwa na nia thabiti ya dhati kuzisaidia nchi zinazoendelea katika kupambana dhidi ya Malaria.
Lengo la kauli mbiyo ya mwaka huu "kupata maendeleo na mafanikio" ni kutokomeza vifo kutokana na malaria ifikapo 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment