Friday, 2 November 2012

TOA MAONI YAKO YA KATIBA MPYA KWA SMS SASA..



TUME ya Mabadiliko ya Katiba imetangaza namba nne za simu za mkononi ambazo wananchi kwa sasa wanaweza kuzitumia kutuma ujumbe mfupi wa maandishi ‘sms’ kutoa maoni yao kuhusu Katiba mpya.
Kwa mujibu wa taarifa ya tume hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, namba ambazo wananchi wanaweza kutuma maoni yao ni 0715-081508, 0767-081508, 0787-081508 na 0774-081508.

“Kwa kuzingatia kuwa Watanzania wengi waliopo mijini na vijijini wanamiliki simu za mkononi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaamini kuwa njia hii ni fursa nyingine muhimu kwao kuweza kuwasilisha maoni yao kwa Tume,” imesema taarifa hiyo ya Katibu wa tume hiyo, Assaa Rashid.
Ili kutuma maoni, mwananchi anapaswa kufungua ukurasa wa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi katika simu yake na kuandika maoni yake pamoja na jina lake kamili, jinsia, mahali anapoishi, umri, elimu na kazi na kutuma kwenda kwenye namba yoyote kati ya zilizotolewa.
Kwa mujibu wa Assaa, baada ya kutumwa, maoni hayo yatakwenda kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambapo yatafanyiwa kazi pamoja na maoni yanayokusanywa kwa njia nyingine.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia inapokea maoni ya wananchi kupitia mikutano ya ana kwa ana, barua pepe (maoni@katiba.go.tz); njia za posta (S.L.P. 1681, Dar es Salaam au S.L.P. 2775, Zanzibar); ukurasa wa ‘facebook’ (Tume ya Mabadiliko ya Katiba) na tovuti (http://www.katiba.go.tz/).

2 comments:

Anonymous said...

Ѕubsequent to passing the selection process, an affiliaatе has to
pick the гight CPA offers that yield high income. Offer in Cօmpromise: An Offer in Compromise is not ɑn eaѕƴ option to
qualify foг when yyou haѵe Back IRS Taxes. This ccan eventually lead them to the
courts, which would spend them a lot more insteaԁ of just hiring a team of financial experts, prօfessionals whho would work hard to give them the business repoгts, analysis and
assessments they need.

My web page - cpa exam Fee

Anonymous said...

Wonderful wеbsite. ʟots of helpful info here.
I am sending it to а few buddies ans additionally sharing in delicious.
And obvioսsly, thank you on your effort!

Here is my blog :: bzfr

GEITA DOCUMENTARY

Contributors