Monday, 29 October 2012

VINARA WA ROCK CITY MARATHONMWANARIADHA anayekuja juu kwa kasi, Mwita Kopiro, wa Mwanza na Mary Naali wa Arusha, jana waliibuka washindi katika mbio za Nusu Marathon za Rock City zilizofanyika jijini Mwanza jana.

Mwita alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume, akitumia saa 1:04:02, huku Mary anayetoka klabu Skytel akishinda kwa wanawake akitumia saa 1:16:33.

Waliofuatia kwa wanawake ni Sarah Ramadhan Arusha (1:16:37), Anastasia Msindai Arusha (1:19:05), Failuna Mohamed Arusha (1:19:20), Musengimana kutoka Rwanda (1:22:09), Banuelia Brighton Holili Kilimanjaro (1:22:15), Dorcas Jepchirchir Kenya (1:26:12), Sarah Kavina JKT Arusha (1:36:37), Furaha Sambeki Tanzania (1:36:55), na Grece Jackson (1:40:53).

Washindi wengine kwa wanaume na muda wao kwenye mabano ni Joseph Chacha, Mara (1:04:03), Alphonce Felix Arusha (1:04:06), Pascal Sarwat Arusha (1:04:11), Amos Limakori Kenya (1:04:23), Keneth Pono Kenya (1:04:25), Elia Daudi Tanzania (1:04:26), Fabiano Joseph Arusha (1:04:57), Stephen Ndege Kenya (1:05:03) huku kumi bora ikifungwa na Patrick Nyangero Arusha (1:05:13).
Dotto Ikangaa kutoka Arusha, aliibuka mshindi katika mbio za kilometa tano wanaume, akimpiku John Joseph kutoka Singida ambaye alishika nafasi ya pili, huku Paul Elias wa Ukerewe, Mwanza akishika nafasi ya tatu.
Jeremiah Kinshuzi wa Mwanza alishinda mbio za kilometa tatu kwa wazee, huku Pascal Emmanuel wa Kisese akishinda kwa watu wenye ulemavu.
Kwa upande wa watoto ambao walikimbia kilometa mbili, Idd Suguta wa Mara na Emma Imhoff wa Singida waliibuka washindi.
Katika mbio hizo, washiriki na mashabiki wake waliburudishwa na msanii maarufu Juma Kassim ‘Sir Nature’ na kundi lake la TMK Wanaume Halisi, akishirikiana na Baby Madaha katika kuuzindua wimbo wao mpya ‘Narudi Nyumbani’ ambao waliimba kwa mara ya kwanza Mwanza.
Rais wa Shirikisho cha Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka, ambaye alikuwa ni mgeni rasmi, licha ya kutoa onyo kwa wavamizi wa viwanja vya michezo, alionyesha kuridhishwa na uratibu wa Rock City Marathon, huku akiongeza kuwa mbio hizi zimeweza kuibua vipaji vingi vya riadha ambayo vinahitaji kukuzwa.
“Nawashukuru sana waandaaji wa Rock City Marathon kwa kuweza kuandaa mashindano, ambayo yameweza kutusaidia sisi wadau wa riadha, kugundua vipaji vingi ambavyo tunavyo hapa nchini ambavyo vinahitaji kukuzwa,” alisema Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Morogoro.
“Hivyo basi natoa wito kwa makampuni, mashirika na hata serikali, kuweza kudhamini mashindano kama haya ambayo yanasaidia sana kuendeleza na kuibua vipaji vya mchezo wa riadha, ambao umeliletea sifa kubwa taifa letu huko nyuma,” alisisitiza Mtaka.
Rock City Marathon ni mbio zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International Ltd tangu mwaka 2009, ambapo kwa mwaka huu zilidhaminiwa na NSSF, Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, ATCL, PPF, African Barrick Gold, New Africa Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).Picha na habari kwa hisani ya Gsengo na freemedia

2 comments:

Anonymous said...

hi vicky-kamata.blogspot.com owner found your blog via search engine but it was hard to find and I see you could have more visitors because there are not so many comments yet. I have found website which offer to dramatically increase traffic to your website http://cheap-mass-backlinks.com they claim they managed to get close to 4000 visitors/day using their services you could also get lot more targeted traffic from search engines as you have now. I used their services and got significantly more visitors to my blog. Hope this helps :) They offer best services to increase website traffic Take care. Richard

Anonymous said...

Thanks for finally talking about > "VINARA WA ROCK CITY MARATHON" < Liked it!

Here is my homepage renovation ideas (www.homeimprovementdaily.com)

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI