Friday, 2 November 2012

MAFUTA BADO UTATAWAKATI Kampuni ya uratibu ya uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PIC) ikipigiana chenga na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kuhusu uhaba wa mafuta nchini, serikali imeagiza kusitisha kusafirisha mafuta nje ya nchi.
Agizo hilo la serikali lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Maswi, alipokutana na Bodi ya PIC pamoja na Ewura mbele ya waandishi wa habari na kuwataka waeleze sababu za kuadimika kwa nishati hiyo nchini.

Maswi alishangaa kuona lita nyingi za mafuta zinazotakiwa kuagizwa nje ya nchi tofauti na ambazo zinatakiwa kuuzwa nchini, ndipo akaagiza hatua ya haraka, nusu ya mafuta yanayotakiwa kupelekwa nje ya nchi yauzwe hapa nchini.
Pia aliagiza PIC kuhakikisha wanasimamia na kuharakisha meli za mafuta kuingia bandarini, huku Ewura wakiagizwa kuchukua hatua za kisheria kwa mfanyabiashara yeyote atakayekiuka taratibu.
Aidha, aliitaka PIC ihakikishe meli tatu ambazo hazijapokelewa katika zabuni ya nne, zinaingiza na kushusha mafuta nchini kabla ya Novemba mosi (leo) kama ilivyokubalika kwenye mkataba wa zabuni hiyo.
“Makampuni ya mafuta (OMCs) yenye akiba ya mafuta yanaagizwa kuwauzia mafuta wamiliki wa vituo vya kuuzia mafuta bila kikwazo chochote,” alisema Maswi.
Katibu Mkuu huyo aliwataka Ewura kuhakikisha inasimamia usambazaji wa mafuta katika maeneo ya mikoani, na kwamba meli ya Mt. Merelina ambayo imebeba tani 14,800 za mafuta ya petroli na diseli 23,700 iliyoanza kazi ya kushusha mafuta jana, yote kupelekwa mikoani.
Mnyika ang’aka
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, alisema kuwa umma upokee kwa tahadhari taarifa zinazotolewa na Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake nje ya Bunge kuhusu masuala ya sekta ya nishati, ikiwemo kuhusu uhaba wa mafuta unaoendelea hivi sasa.
Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), alimtaka Spika wa Bunge, atoe maelezo bungeni ya kuelekeza Kamati ya Kudumu ya Bunge itakayochambua ukweli wa taarifa hizo na pia kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu masuala husika.
Alisema kuwa, kujirudia mara kwa mara matatizo katika sekta za nishati, hususan katika biashara ya mafuta, kumechangiwa na sababu za udhaifu wa kisera, kimaamuzi, kiusimamizi na kiutendaji wa baadhi ya viongozi na watendaji.
“Hata hivyo, katika kipindi hiki cha Oktoba, ni matokeo ya Wizara ya Nishati na Madini na Ewura kukosa chombo cha kusimamia kwa karibu mamlaka hizo kwa niaba ya wananchi baada Kamati ya Nishati na Madini kuvunjwa, na Spika kuacha kuelekeza kamati mbadala ya kudumu ya Bunge ya kushughulikia masuala ya haraka ya nishati,” alisema.
Mnyika aliongeza kuwa, kutokana na matatizo yaliyopo kwenye sekta ya nishati, na kwa kuzingatia kuwa mamlaka na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa katiba ni kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi, alimwandikia barua Spika wa Bunge ili Wizara ya Nishati na Madini iwajibike kueleza hali halisi.

2 comments:

Anonymous said...

Phen375 (Phentemine375) is really an innovative new merchandise that is gaining
interest as a additional fat burner. Phen 375 fat
loss medications include things like phentemine,
a program in which performs equally as being an hunger controller along with a extra fat burner.
buy phentermine onlinegoing on a diet
organic remedy is authorized because of the Federal drug administration
as well as is manufactured out of the best parts. There's a chance you're hesitant toward
diet approach remedies when you have used almost every little thing only
to eliminate fat, nonetheless would not find beneficial benefits.
Bodyweight surplus fat can be quite a overwhelming process.

However this fresh fat burning guide might be really worth a go.
The following ideal weight decline health supplement seriously isn't just validated to get powerful, it gives an on the net service collection to manual people each and every stage. Phen 375 is known as any safe way to get rid of fat. Phen375 besides adjustments your cravings, it can also help you actually keep a higher level of one's to enable you to melt off much more calorie consumption.
Along with changing the landscape of indicates such as Most important Loser, you may have found that you'll want to eat so that you can lose weight. The majority of men and women usually go overboard regarding skipping meals or feeding on a lesser amount of to lose weight naturally. You dont get rid of whatever you don't have.
What exactly Phen375 is actually it retains your current metabolic rate
higher and that means you are able to afford melt off that which you eat.
Here is my blog ; how to lose weight easily

Anonymous said...

Eҳcellent article. I certainly love this site. Continue the good work!


Ӎy page :: Get Thin

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI