Wednesday, 8 August 2012

Watoto wa mitaani watishia usafi Moshi

HALMASHAURIA ya Manispaa ya Moshi inakabiliwa na ongezeko la watoto wa mitaani wanaotishia kuibuka kwa vitendo vya uhalifu, huku mashirika ya Serikali na yasio ya Serikali yakitakiwa kusaidia kutoa elimu na ajira.
 
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Bernadette Kinaboalisema halmashauri ina hofu baada ya ongezekola watoto wa mitaani,hali inayoweza kusababisha kuongezeka kwa vitendo vya ujambazi na magonjwa ya maambukizi. 


Kinabo alisema mwaka 2009 Manispaa ya Moshi ilikuwa na watoto wa mitaani 4,600, ambao walitoka familia za ndoa zilizovunjika ikiwamo umaskini uliowaondoa majumbani kwa kukosa huduma muhimu. 
Alisema zaidi ya nusu watoto hao wanasomeshwa na taasisi zisizo za Serikali na wengine wanasomeshwa kupitia magari (Mobile School ), badala yake wamekuwa wakirejea mitaani na kujitumbukiza katika vitendo viovu na uporaji. 

“Kwa kweli kila siku ziendavyo halmashauri inazidi kukabiliwa na ongezeko la watoto wa mitaani licha ya mji wetu kuwa msafi, wamekuwa wachafuzi wakubwa kwa baadhi ya maeneo,” alisema Kinabo.

Kuhusu usafi wa mji huo, Kinabo alisema tangu mwaka 2006 ilipoweka sheria ndogo ya usafi wa mazingira ikisaidiana na sheria ndogo ya ada na ushuru ya mwaka huohuo, wamekuwa na mafanikio makubwa wa kuuweka mji wa Moshi katika hali ya usafi wa hali ya juu. 

Alisema mji huo umekuwa wa kwanza kwa usafi katika halmashauri 17 nchini kwa miaka mitano mfululizo, hivyo kuwafanya wageni wakiwamo watalii kutembelea mara kwa mara ikiwamo maeneo ya vivutio. 

Alisema hali hiyo imesababisha kutoa ajira kwa vikundi vya jamii na kupata ufadhili kutoka mji wa Delray Beach, nchini Marekani na kwamba, karibu watawasili hivi karibuni kuimarisha vikundi kazi kupitia mradi wao wa Manispaa ya Moshi. Habari kwa hsani ya Mwananchi comm. 

No comments:

GEITA DOCUMENTARY