Wednesday, 8 August 2012

Vifo vya wajawazito, watoto vyakithiri Kigoma


MKOA wa Kigoma unakabaliwa na changamoto ya vifo vya wajawazito na watoto wa chini ya miaka mitano kwa sababu wajawazito wengi hujifungulia majumbani.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) Dk. Leonard Sumbi alisema hayo wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya afya ya mkoani hapa uliokuwa ukijadili mkakati wa kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wa chini ya miaka mitano.

Dk. Sumbi alisema zaidi ya asilimia 42 ya wajawazito mkoani hapa wanajifungulia majumbani na kina mama hao hufariki kutokana na kuchelewa kufikishwa hospitali wanapopata matatizo wakati wa kumpata mtoto.

Alisema suala la uchache wa watumishi katika sekta ya afya na miundombinu duni ya usafiri katika maeneo mbalimbali hasa vijijini husababisha kinamama kushindwa kufika kwa wakati katika vituo vya kutolea huduma za afya jambo linalochangia vifo vya wajawazito.

Kuanzishwa kwa huduma za upasuaji katika vituo 12 vya afya vya mkoani hapa kulikofanywa kupitia ufadhili wa taasisi ya Word Lung Foundation kumesaidia kukabiliana na tatizo la vifo vya wajawazito wakati wa kujifungia kwa sababu vitawezeshwa kutoa huduma bora zaidi ikiwemo upasuaji pale inapohitajika.

No comments:

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI