Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema, meli iliyozama jana katika kisiwa cha Chumbe, Zanzibar ilikuwa na abiria 248 wakiwemo watoto 31.
Kwa mujibu wa Sumatra, meli hiyo, inamilikiwa na Kampuni Seagul Transport, imasajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na kwamba, Cheti cha Ubora kimeanza tarehe 24 Agosti, 2011 na kinamalizika 23 Agosti, 2012. Imesema, meli hiyo ilikuwa imeruhusiwa kubeba abiria wanaoruhusiwa 300 na tani 26 za mizigo.
SUMATRA kupitia Kituo cha Utafutaji na Uokoaji (MRCC) ilipata taarifa kuwa meli ya MV Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar ilikuwa inazama katika eneo la karibu na kisiwa cha Chumbe, Zanzibar, eneo ambalo lipo umbali wa Kilomita za Bahari 13.8 kutoka Bandari ya Zanzibar.
Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kutoka kwa Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I, Police Patrol Boat, Navy.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali.
Meli ya Mv Skagit ikiwa imeshazama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250 juu ni baadhi ya waokoaji wakiwa tayari kutoka huduma ya kwanza
Mwokoaji akiwa na mmoja wa maiti wa ajali hiyo
Waokoaji wakiokoa moja ya maiti. wakiwa katika boti ya Kilimanjaro.
Majeruhi wakiwa katika mgongo wa boti hiyo wakisubiri kuokolewa.
Baadhi ya Abiria wakiwa katika moja ya chombo cha kuokolea wakielea baharini kusubiri kuokolewa.
Boti ya KMKM ikiwa katika zoezi la kuokoa majeruhi.
PICHA KWA HISANI YA MJENGWA BLOG .
No comments:
Post a Comment