Thursday 19 April 2012

MAOMBI YA KUPANDA KWA NAULI ZA DALADALA YATINGA SUMATRA


CHAMA cha Wamiliki wa Daladala MKoa wa Dar es SAlaam (DACOBOA)wamepeleka maombi yao Mamlaka ya Udhibiti Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kwa ajili ya kuongeza bei mpya ya nauli za daladala.
Maombi hayo ya kuongeza bei ya nauli mpya yametokana na madai ya wamiliki wa daladala Dar es Salaam kwamba  gharama za uendeshaji zimepanda.

Akizungumza Dar es Salaam jana,Mwenyekiti wa DACOBOA Bw.Sabri Mabrok alisema kuwa wamepeleka maombi hayo SUMATRA ili yaweze kufanyiwa kazi.

"Mapendekezo ya bei mpya tumeshakabidhi kwa SUMATRA tunasubiria hatua za utekelezaji kwa sababu na bei za vifaa pamoja  na gharama zingine za uendeshaji zipo juu sana kwa sasa."alisema Bw.Mabrouk.

Alielezea bei za uendeshaji zilivyokuwa kwa  mwaka 1995 ambapo ziko tofauti na za sasa.

Alisema  bei ya mafuta lita moja ilikuwa ikiuzwa sh.385 na bei ya nauli ya daladala sh. 150 na kwa upande wa dola moja ilikuwa sh.1600, lakini sasa hivi bei ya lita moja sh. 2200 wakati dola moja inauzwa kwa sh.1900.

Kwa upande wa bei ya  taili moja shilingi 400,000 na bei ya betri la gari 150,000 ambapo mwaka 1995 betri la gari lilikuwa likiuzwa kwa sh.70,000.

Alisema kuwa sababu kuu za kuomba kupandisha gharama za nauli  ni kutokana na mbiundombinu kuwa mibovu na sababu hizo hapo juu,pamoja na  kuharibika kwa magari yao ambapo asilimia 100 ya daladala  na vituo vyote vibovu pia.

"Tumeshindwa kupandisha bei kiholela ya daladala kutokana na  daladala hazipo katika biashara huria ndio maana tumefuata sheria kupitia ngazi husika hatuna mamlaka ya kupandisha bei tofauti biashara nyingine za mmiliki kuamka asubuhi na kutoa bei ya bidhaa yake.

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors