SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) limesema hakuna tatizo la nishati hiyo kwa wakazi wa Dar es Salaam na viunga vyake, baada ya kutengemaa kwa kituo kidogo cha usambazaji (substation) cha Upanga.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, alisema umeme hukatika mara kwa mara hususan maeneo ya Kimara ambako wakazi wake wanalilalamikia shirika hilo.
Aliwataka wakazi wa jijini hapa kuamini kwamba hakuna tatizo la umeme huku akibainisha kuwa kituo cha usambazaji kilichokua kikifanyiwa marekebisho cha Upanga kimetengemaa.
“Baadhi ya maeneo hasa Upanga na katikati ya jiji palikuwa na tatizo la umeme kwa sababu ya hitilafu kidogo kwenye ‘substation’ ya Upanga lakini sasa imerekebishwa hakuna tena tatizo. Mitambo yote inayozalisha umeme na iko kwenye hali nzuri ila kwenye hizo substation ambazo zinapokea na kusambaza umeme wakati mwingine zinaleta taabu lakini kwa sasa hakuna tatuzo,” alisema Badra.
No comments:
Post a Comment