Friday 15 July 2011

MAELFU WAKIMBIA MASHAMBULIO YA NIGERIA

Maelfu ya raia wa Nigeria wanakimbia eneo la Maiduguri kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kufuatia mashambulio ya hivi karibuni, yaliyoua takriban watu 40.

Baadhi yao ni wanafunzi wakiondoka baada ya chuo kikuu kufungwa.
Askari karibu na eneo lilipotokea mlipuko
Mashambulio hayo yamefanywa na kundi lenye msimamo mkali, Boko Haram, linalopinga elimu ya kimagharibi.
Majeshi ya usalama yameshutumiwa kufyatua risasi ovyo na kuua raia.
Boko Haram limefanya mashambulio yao mengi Maiduguri lakini pia limelipua mabomu kwenye mji mkuu, Abuja, katika miezi ya hivi karibuni.
Mwandishi wa BBC Bilkisu Babangida akiwa Maiduguri alisema mji huo umegubikwa na hofu huku wengi wakiwa wamejifungia ndani.
Waandishi wanasema vituo vya mabasi vimejaa watu tele huku harakati za watu kuondoka zikiongezeka.
Baadhi ya watu wameondoka kwa miguu wakiwa na vitu vyao na mifugo.
Siku ya Jumanne asubuhi, wanajeshi wa kufanya doria walilengwa huko Maiduguri na katika hali ya kutaharuki, watu wanne walipigwa risasi na kufa huku wanajeshi wawili wakijeruhiwa.
Pia kumekuwepo na mlipuko kwenye kanisa mjini Seluja, karibu na mji mkuu, Abuja.
Hakuna taarifa zozote za vifo katika tukio hilo.

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors