Friday 15 July 2011

WAFANYAKAZI WA BBC KUGOMA

Waandishi habari wengi wanaohudumu katika Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC wameanza mgomo wa siku moja kulalamikia mpango wa kuwaachisha kazi baadhi yao.

Hii inafuatia hatua ya serikali ya Uingereza kupunguza matumizi yake katika sekta ya umma.Wasimamizi wa BBC wamesema hatua ya kuwapunguza wafanyakazi haingeweza kuepukika.
Miongoni mwa idara zilizolengwa ni Idhaa ya dunia pamoja na ile inayofuatilia matangazo kote duniani. Muungano wa chama cha waandishi habari NUJ umesema mgomo wa leo unawashirikisha watangazaji wa shirika la BBC kote duniani. NUJ imesisitiza kwamba hatua ya kupunguza wafanyikazi haifai kamwe.

Mgomo wa leo Muungano huo unasema utavuruga matangazo ya habari za idhaa ya BBC. Mgomo huu unafuatia hatua ya BBC kuwaachisha kazi wafanyika wake katika Idhaa ya Dunia{ BBC World Service} pamoja na idara inayofuatilia habari za dunia{ BBC Monitoring}.

Katibu Mkuu wa Muungano wa chama cha waandishi habari Michtell Steintrit, amesema NUJ imeweka masharti ya kutowaachisha kazi wafanyikazi wa BBC kwa misingi kwamba huduma zao hazihitajiki.

Amesema mzozo wowote kuhusiana na utendakazi wa waandishi habari unafaa kujadiliwa na pande zote akisema ombi hilo lilipuuzwa na wasimamizi wa BBC.
Kwa upande wao wasimamizi wa BBC wamelazimika kuwaachisha kazi wafanyikazi 397 kwenye Idhaa ya Dunia na ile inayofuatilia habari za dunia kuufuatia mpango wa serikali wa kupunguza bajeti yake katika sekta ya Umma.

BBC inasema wengi waliosimamishwa kazi ilikuwa kwa hiari, baadhi wakahamishiwa maeneo mengine lakini mia moja wakalazimishwa kustaafu. Mpango huo iliwalenga wafanyikazi wote ambao ni wachama na wasio wachana wa muungano wa chama cha NUJ.

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors