Thursday, 16 March 2017

VICTORIA FOUNDATION YATILIANA SAINI NA YAMOTO BAND KATIKA KUFANIKISHA PROGRAM YA "FOR THEM"

Na Steven Mruma


       Leo mkurugenzi na mwenyekiti wa Victoria Foundation ametiliana saini mkataba wa pamoja wa kuanikisha program maalum ya  "FOR THEM" na kundi la muziki wa kizazi kipya la Yamoto Band. Mkataba huo utawezesha kuhamasisha na kufanikisha program maalum kwa ajili ya watoto yatima wajane pamoja na waemavu. Mkataba huo umetiwa saini Jijini Dar es salam katika ofisi zaVictoria Foundation kati ya mwenyekiti wa Victoria Foundation na mbunge wa viti maalum mkoa wa Geita Mh. Vicky Kamata Likwelile na Kiongozi wa Yamoto Band.





Saturday, 11 March 2017

VICTORIA FOUNDATION YAGAWA MASHUKA 100 HOSPITAL YA MKOA WA GEITA


Tarehe 10.03.2017
Mhe Vicky Kamata Likwelile Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Geita amefanya ziara na kugawa mashuka 100 katika hospitali ya Mkoa wa Geita kwenye ward ya akina mama na watoto,
Aidha Mhe Vicky Kamata Likwelile amesikiliza changamoto mbalimbali za wagonjwa ikiwemo tatizo la upungufu wa vitanda pamoja na ward za akinamama.
Lakini pia amesikiliza changamoto mbalimbali toka kwa watumishi wa hospital hiyo ikiwemo suala la uchache wa wahudumu wa afya na Madaktari ikiwemo madaktari wa magonjwa ya akina mama na watoto.
Mhe Vicky Kamata Likwelile ameahidi kuzifanyia kazi changamoto hizo.
Katika ziara hiyo ya Mhe Vicky Kamata Likwelile aliambatana na viongozi wa wa UWT akiwemo Mhe Maimuna Mingisi (DV) Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Geita na Ndugu Mazoea Salum Katibu wa UWT Wilaya ya Geita.
Mhe Vicky Kamata amewashukuru madaktari na wauguzi wa Hospitali hiyo na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanazofanya za kuwahudumia wagonjwa.
Imetolewa na
Mazoea Salum
Katibu wa UWT
Wilaya ya Geita
Imehaririwa na Steven Mruma Jr.






Friday, 10 March 2017

MH. VICKY KAMATA APOKEA TUZO YA HESHIMA KWA KUPIGANIA HAKI ZA WANAWAKE

Na Steven Mruma 

   Mh. Vicky Kamata Likwelile amepokea tuzo ya heshima kwa kutambulika kwa mchango wake mkubwa alio uonyesha kwa jamii ya wanawake wa Tanzania na kanda ya ziwa kwa kupitia nafasi zake aizonazo kama Mbunge, lakini pia kama mwanamuziki hasa kupitia wimbo wake wa "Wanawake na Maendeleo" na pia kupitia tasisi yake ya Victoria Foundation. 
   Tuzo hizo zimetolewa na NITETEE WOMAN AWARD hafla iliyofanyika jijini mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wanawake akiwemo naibu waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi Angeina Mabula









GEITA DOCUMENTARY

Contributors