Monday, 18 August 2014

PICHA: MAMA TUNU PINDA ALAKIWA BAADA YA KUREJEA KATIKA MTANO WA WAKE WA MAWAZIRI WA KUU AMBAPO ALITUNUKIWA TUZO YA HESHIMA KAMA BALOZI WA AMANI DUNIANI

Picha Habari na Steven Mruma "Trust"  
       Ilikua ni mapokezi ya aina yake ya kumpokea moja kati ya wanawake mashujaa ambaye ni mke wa waziri mkuu wa Tanzania mama Tunu Pinda alipokua kwenye mkutano wa dunia kuhusu mambo ya ya amani na kutunukiwa cheti cha kumtambua kama Balozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika hivi karibuni (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini.
 
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas Walsh (kushoto) na Mwenyekiti wa UPF, Dk. Charles Yang mara baada ya kutunukiwa cheti cha kumtambua kama Balozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama  uliofanyika Seoul Korea Kusini.
      Baada ya kutunukiwa tuzo hiyo kama balozi wa amani na usalama duniani Mama Tunu pinda aliwasili nchini na kufanyiwa mapokezi makubwa na baadhi ya viongozi wanawake pamoja na mumewe waziri mkuu wa Tanzania Mizengo K.P. Pinda.
     Miongoni mwa waliompokea alikuwepo mbunge wa Viti maalum na mpambanaji wa haki za wanawake duniani Mh. Vicky Kamata pamoja  na wanaharakati na viongozi mbalimbali wanawake.

ANGALIA PICHA ZA MAPOKEZI YAKE J.K.NYERERE INTERNATIONA AIRPORT ALIPOWASILI
No comments:

GEITA DOCUMENTARY