Tuesday, 16 December 2014

PICHA: PIGO CHADEMA: WANACHAMA ZAIDI YA 35 BAWACHA WAHAMIA CCM GEITA BAADA YA KUCHOSHWA NA UBABAISHAJI WA CHAMA HICHO.

 Na Steven Mruma
       Hivi karibuni wakati wa kampeni za uchaguzi kikundi cha akina mama zaidi ya 35 wa BAWACHA kutoka chama cha Chadema, waliamua kukikimbia chama hicho na kukimbilia kwa Baba na Mama aliyewalea CHAMA CHA MAPINDUZI baada ya kuchochwa na sera chafu na ubabaishaji wa chama hicho cha Chadema.
      Mara baada ya kukutana na Mh. Vicky Kamata wakati akiendelea na kampeni za kuwanadi wagombea wa serikali za mitaa Geita walimueleza kuwa sasa wanajiskia amani kurudi nyumbani baada ya kukichoka chama hicho walichokikimbia cha Chadema. 

Baadhi wa waliokuwa wakina mama kutoka chama cha chadema Bawacha waliohamia CCM wakimueleza jinsi walivyoishi katka shida nyingi wakati wakikitumikia chama cha chadema

Baada ya kurudisha kadi za Chadema Mh. Vicky Kamata aliwakabidhi kadi za CHAMA CHA MAPINDUZI

Mh. Vicky akiwa na wanachama wa CHAMA CHA MAPINDUIZI mara baada ya kuwakabidhi kadi za CCM wakinamama waliokihama chama cha chadema na kuhamia CCM

Baadhi wa waliokuwa wakina mama kutoka chama cha chadema Bawacha waliohamia CCM baada ya kukabidhiwa kadi za CCM na Mh. Vicky Kamata.

1 comment:

Anonymous said...

wanajipendekeza hao ili wagawiwe vitenge na chunvi hawana jipya

GEITA DOCUMENTARY