Ilikua ni siku ya ijumaa tulianza safari kuelekea Nyamisati rufiji mkoani Pwani kwa ajili ya maandalizi ya mahafali ya Shule ya sekondari ya wama nakayama.
tuliwasili jioni na kupokelewa na uongozi wa shule na kukaa pamoja kujipanga na maandalizi ya ya mahafali hayo.
Jioni ya Ijumaa tuliwasili Nyamisati |
na Tulishuhudia mandahri nzuri ya sule ya Wama nakayama ilivyo safi na nzuri |
mandhari ya shule na kwa mbali wanafunzi wakiendelea na usafi |
baadhi ya majengo ya madarasa |
eneo lingine la madarasa |
Mh. Vicky kamata akisaini kitabu cha wageni |
kushoto ni Mkuu wa Shule ya Wama nakayama wakijadili namna ya kujipanga na maandalizi ya mahafali. |
usiku ulipoingia wanafunzi walikutana eneo la bwalo na tulianza na mazoezi ya nyimbo na kucheza yakiongozwa na Mh. Vicky |
Kesho yake asubui tuliamka mapema na tuliwakusanya wanafunzi na kuafanya mazoezi kwa siku ya pili |
wakati tunasubiria wanafunzi watoke breakfast tulikua tunapewa mawaidha na Mh. Vicky Kmata na hapa ilikua zamu yangu. |
muda wa mazoezi ulifika na mazoezi yalizna kama kawaida. |
Mh, Vicky akifatilia kwa karibu mazoezi |
mazoezi yakiendelea. |
hapa alijumuika nao na alionyesha namna gani yuko vizuri kwa kucheza na sio kwa kufundisha tu |
ilikua ni burudani kwa sisi waangaliaji |
baada ya mazoezi tuliamua kutembelea kijiji cha Nyamisati na hapa tulikua tunapata Ugali mlenda samaki na maharage. |
pamoja na meza kuchafuka kwa misosi lakini gharama zote zilikua 6000/= tu |
msosi ukiendelea |
baada ya msosi tulienda kijiwe cha madafu kushushia |
hapa tulitaka kuvuka mto huu kuelekea kijiji jirani beach lakini daah niligoma sipendi sana kusafiri majini |
majadiliani yakiendelea jinsi ya kwenda beach mimi nilizidi kuweka mgomo baridi |
tukaamua kurudi kijiwe cha madafu na kuendelea na kazi ya kunywa madafu |
mzee muuza madafu akiendelea kutuhudumia |
na jioni tuliamua kutafta sehemu ya kupunzika na tuliendelea kujadili mambo mbalimbali kusubiri siku ya mahafali yaani siku inayofatia. |
No comments:
Post a Comment