Monday, 27 October 2014

PICHA ZA MAHAFALI NYINGINE YA KIHISTORIA SHULE YA WAMA NAKAYAMA.. MH VICKY AKONGA NYOYO ZA WALIOHUDHURIA KWA SHOO KALI NA WAHITIMU, WAGENI WAALIKWA WASHUKA JUKWAANI KUCHEZA WAKIONGOZWA NA DR. ASHA ROSE MIGIRO NA MAMA SALMA KIKWETE.


Na. Steven Mruma, Nyamisati Rufiji.
 
    Shule ya sekondari ya Wama nakayama tar 26/10/2014  ilifanya mahafali yake ya pili tangu kuanzishwa kwake. katika mahafali hayo mgeni Rasmi alikua ni Dr. Asha Rose Migiro ambaye pia aliambatana na viongozi Mbalimbali akiwemo mke wa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete pamoja  na Waziri wa Afya Seif Rashid,  Joel Bendera ambaye ni mkuu wa mkoa wa Morogoro. Mh Hawa Ghasia waziri wa TAMISEMI. pia alikwepo Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada na viongozi wengine wengi..
    Katika mahafali hayo pia walikiwepo wasanii mbalimbali akiwemo Mrisho Mpoto na Mjomba Band na Pia Mh. Vicky Kamata ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Geita. Mara tu baada ya mahafali kuanza wahitimu wakiongozwa na Mh. Vicky Kamata waliimba wimbo maalum ambao ulikonga vilivyo nyoyo za wageni waalikwa ikiwemo meza kuu na bila ajizi walijikuta wakiiacha meza kuu na kushuka jukwaani na kuanza kucheza pamoja na wahitimu na walimu na wageni wengine waalikwa. Na wote walionyesha ustaadi mkubwa wa kucheza si Mama Salma wala Dr. Asha Rose Migiro wala Balozi wa Japan Masaki Okada wote walionyesha ujuzi wa hali ya juu ya kucheza pamoja na wahitimu na wageni wengine waalikwa.
    Ikumbukwe pia kua Mh. Vicky Kamata ni msanii aliyewahi kutamba na kibao cha wanawake na maendeleo, mapenzi na shule, Fitina, Sikumbuki kuku, nimeolewa na pia kwasasa anatamba na kibao chake cha Moyo wa mtu kichaka, Wimbo ambao pia unabeba jina la Albam yake mpya itakayoingia sokoni mwishoni mwa mwaka huu.

 Zifuatazo mi baadhi ya picha za mahafali hayo ya kihistoria.


SEHEMU ILIYOANDALIWA KWA AJILI YA MAHAFALI MAPEMA ASUBUHI SIKU YA MAHAFALI

MITAMBO IKIWEKWA SAWA NA MJOMBA BAND

MEZA KUU IKIWA IMEPAMBWA VIZURI

MANDHARI NZURI YA SHULE NA KWA MBALI WANAFUNZI WAKINDELEA NA MAJUKUMU MAPMA KABLA YA MAHAFALI KUANZA.

ENEO LA JENGO LA UTAWALA

SEHEMU AMBAYO ILITENGWA KWA AJILI YA MAHAFALI IKIWA NADHIFU KABISA.

MH. VICKY AKIFURAHIA JAMBO WAKATI WA MAZOEZI YA MWISHO ASUBUI KABLA YA MAHAFALI

WAHITIMU WAKIFANYA MAZOEZI YA MWISHO KABLA YA MAHAFALI

MAZOEZI YAKIENDELEA

MARA BAADA YA MAZOEZI MJOMBA MPOTO ALIKUTANA NA SHWAHIBA WAKE NA KUPATA PICHA YA PAMOJA

MRISHO MPOTO KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MTUMISHI PAUL MSYANGI AMBAYE PIA TULIKUA NAE KATIKA MSAFARA WA MH. VICKY

PAMOJA KUWA MDA MWINGI NIPO NYUMA YA CAMERA NILIPATA SHAVU LA PICHA NA MJOMBA.
WAGENI WAALIKWA NA WANAFUNZI WANAOBAKI AU WAAGWA WAKIWA TAYARI WAMEWASILI KWA WINGI SANA KUSHUHUDIA MAHAFALI YA PILI YA WAMA NAKAYAMA.

HAPA KIBAO CHA WANAWAKE NA MAENDELEO KIKIPIGWA NA WANAWAKE WENGI WALISHINDWA KABISA KUJIZUIA NA KUNGANA KUCHEZA PAMOJA  WAKIONGOZWA NA MH. VICKY KAMATA
JUA NA JOTO LILIKUA KALI SANA NILIAMUA KUPUNZIKA NA KUENDELEA KUSHUHUDIA BURUDANI MBALIMBALI NA PEMBENI AKIONEKA MH. VICKY AKIWA NA UCHOVU HASA IKIZINGATIA HAKUA VIZURI KIAFYA KWANI ALIKUA ANASUMBULIWA NA MAFUA

BURUDANI ZA NGOMA ZIKIENDELEA

WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO WAKIONYESHA UWEZO MKUBWA WA KUCHEZA NA KUTOA BURUDANI YA AINA YAKE.

MAMA SALMA KIKWETE AKIWA ENEO LA KITUO CHA AFYA AKISUBIRI KUWASILI MGENI RASMI KUFUNGUA KITUO HICHO CHA AFYA CHA SHULE


MGENI RASMI DR. ASHA R. MIGIRO KATIKATI AKIWA TAYARI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA UFUNGUZI WA KITUO CHA AFYA CHA SHULE YA WAMA NAKAYAMA. KUSHOTO NI MKE WA RAIS WA TANZANIA MAMA SALAMA KIKWETE NA KULIA NI BALOZI WA JAPAN NCHINI MASAKI OKADA NA ANAYEONEKANA KWA MBALI KULIA NYUMA YA BALOZI WA JAPAN NI WAZIRI WA AFYA SEIF RASHID

MGENI RASMI AKICHUKUA MKASI KUKATA UTEPE IKIWA NI ISHARA YA KUFUNGUA KITUO HICHO AKIWA PAMOJA NA MAMA SALAMA KIKWETE NA BALOZI WA JAPAN NCHINI MASAKI OKADA
BAADA YA UFUNGUZI WA KITUO WAGENI WALIWASILI ENEO LA MAHAFALI NA KUPOKELEWA KWA SHANGWE
WANAFUNZI WANAOHITIMU WAKIANDAMANA KUELEKEA ENEO LA MAHAFALI
WAHITIMU MARA BAADA YA KUWASILI ENEO LA MAHAFALI NA HAPA WAKIWA TAYARI KUIMBA WIMBO WA TAIFA NA WIMBO WA SHULE
BENDI YA WANAFUNZI IKIWAONGOZA WAHITIMU WANAFUNZI NA WAGENI WAALIKWA KUIMBA WIMBO WA TAIFA NA WIMBO WA SHULE

MARA BAADA YA WIMBO WA TAIFA NA WIMBO WA SHULE RATIBA ILIENDELEA NA HAPA WANAFUNZI NA WAGENI AKIWEMO MH.VICKY WAKIFATILIA KWA MAKINI

MUDA WA WIBO MAALUM WA WAHITIMU WULIWADIA NA HAPA WAHITIMU WAKIJIPANGA TAYARI KUANZA KUIMBA WIMBO HUO
WAHITIMU WAKIONGOZWA NA MH. VICKY KAMATA WAKIWA TAYARI KUANZA KUIMBA WIMBO MAALUM WA WAHITIMU

ILIKUWA NI WIMBO WENYE HISIA KALI SANA MARA TU UNAPOANZA HASA IKIZINGATIA WAHITIMU HAWA WOTE NI YATIMA

NA SASA WIMBO ULIANZA KUCHANGAMKA NA WAHITIMU WOTE WALISAHAU KUWA NI YATIMA KWA MAANA WALIPATA MAMA WA KUWALEA YAANI MAMA SALMA KIKWETE NA HAPA WALIKUA WAKIMUITA KUMPONGEZA JAPO KWA MAUA

MAMA SALMA ALISHUKA JUKWA KUU NA KUJA KUPOKEA ZAWADI HIYO NA ALISHINDWA KUREJEA JUKWAA KUU NA KUANZA KUCHEZA PAMOJA NA WAHITIMU HAO KWA FURAHA.

MAMA SALMA AKIONYESHA UWEZO MKUBWA WA KUCHEZA NA KWA NYUMA VICKY KAMATA NA WAHITIMU WALIENDELA KUSHUSHA BURUDANI

UZALENDO ULIWASHINDA WENGI HATIMAYE MGENI RASMI NA MEZA KUU NAO WALIJIKUTA WAKIWA MIONGONI MWA WAHITIMU NA WALIMU WA SHULE YA WAMA NAKAYAMA WAKICHEZA PAMOJA KWA FURAHA NA KILA MMOJA ALIONYESHA UJUZI WAKE WA KUCHEZA.

BURUDANI IKIENDELEA NA HATA BAADA YA HITILAFU YA UMEME MH. VICKY ALIENDELEA KUIMBA PAMOJA NA WAHITIMU BILA VYOMBO NA WAGENI WAALIKWA WALIENDELEA KUCHEZA

BALOZI WA JAPAN MASAKI OKADA ALIKIONYESHA UFUNDI WA KIJAPAN KUCHEZA HUKU AKIWA AMEMSHIKA MKONO MAKAMU MWENYEKITI WA BODI YA SHULE YA WAMA NAKAYAMA MH. ZAKIA MEGHI

BURUDANI IKIENDELEA
MARA BAADA YA HITILAFU YA UMEME KUA SAWA WIMBO ULIOMBWA KURUDIWA NA WAHITIMU WAKIONGOZWA NA MH. VICKY WALISHUSHA TENA BURUDANI.

BURUDANI IKIENDELEA

NA SAFARI HII JAPOKUWA MEZA KUU HAWAKUSHUKA TENA ILA WALISHINDWA KUKAA WALIJIKUTA MDA WOTE WAKIFURAHIA NA KUFATISHA BURUDANI HIYO

SEHEMU YA VIONGOZI WA BODI YA SHULE WAKIFATILIA BURUDANI YA WAHITIMU

WAHITIMU WAKIOGOZWA NA MH. VICKY WAKIONYESHA UWEZO MKUBWA WA KUCHEZANA



MARA BAADA YA BURUDANI KUISHA TULIANZA SAFARI YA KUREJEA DAR ES SALAM IKUMBUKWE KUA AFYA YA MH. VICKY HAIKUA VIZURI IJAPOKUWA AIJIKAZA NA KUTOA BURUDANI YA AINA YAKE. NA NJIANI TULIKUTANA NA AJALI MBAYA YA GARI NA MPAKA TUNAONDOKA MAHALI  HAPA HAKUNA KIFO KILICHORIPOTIWA JUU YA AJALI HII LAKINI KULIKUA NA MAJERUHI WATATU NA WALISHAWAHISHWA HOSPITALI

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors