Mwishoni mwa mwezi wa August 28/29, niliandika makala ikizungumzia mtoto aitwaye Ester aliyekua anaugua kansa na kupelekea kukatwa mguu wake..
Pamoja na kufanikiwa kupunguza makali ya kansa lakini tulishachelewa kansa ilimuathiri sana na kusababisha hitilafu katika mapafu yake hali iliyopelekea kufariki dunia mnamo tarehe 18/09/2014 na kuzikwa tar 20/09/2014 jijini Dar es salam.
Pamoja na kupitia maisha ya maumivu kwa takribani miaka miwili baada ya kukutana na Victoria foundation Ester na familia ikiwemo watendaji wa Victoria foundation tuliamini kama Ester angepona na kuishi tena maisha ya furaha, japo haikua hivyo tunaamini ilikuwa ni mpango wa MUNGU hadi hapo hitimisho la Ester lilipotimia, yaani mauti yake.
sipendi kulizungumzia sana hasa kutokana na makala niliyowahi kuandika katika Blog hii mwishoni mwa mwezi wa August.
Tumia muda mchache kuangalia picha za tukio la mazishi yake yaliyofanyika jijini Dar es salam wikend iliyopita.
MWILI WA MAREHEMU UKITOLEWA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI HOSPITALI YA AMANA |
MWILI UKIPANDISHWA KWENYE GARI KUELEKEA NYUMBANI KWA AJILI YA MAZISHI |
MWILI WA ESTER UKIWA NYUMBANI TAYARI KWA KUAGWA |
MTUMISHI WA MUNGU AKIONGOZA MISA YA KUMUAGA MAREHEMU ESTER |
MWILI WA ESTER UKIAGWA NA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI |
ILIKUA NI VILIO NA SIMANZI NA WENGINE WALIDHIRAI MARA BAADA YA KUONA MWILI WA MAREHEMU ESTER |
DEOGRATIAUS MOJA KATI YA VIONGOZI WA VICTORIA FOUNDATION AKIAGA MWILI WA MAREHEMU |
STEVEN MRUMA MWANDISHI WA MAKALA HII NA MAKALA MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA VICTORIA FOUNDATION AKIAGA MWILI WA MAREHEMU. |
ALPHA MOJA KATI YA VIONGOZI WA JUU WA VICTORIA FOUNDATION AKIAGA MWILI WA MAREHEMU ESTER |
NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WAKIAGA MWILI WA MAREHEMU |
MWILI WA MAREHEMU ESTER UKIPANDISHWA KWENYE GARI KUELEKEA MAKABURINI KWA AJILI YA MAZISHI |
MWILI WA ESTER UKIWA MAENEO YA MAKABURINI NA HAPA NDIPO ALIPOLALA KATIKA NYUMBA YA MILELE. |
MWILI WA ESTER UKIWEKWA KABURINI |
MWILI WA ESTER UKIFUKIWA[UKIZIKWA] KABURINI |
WAWAKILISHI WA VICTORIA FOUNDATION STEVEN MRUMA NA ALPHA WAKIONGOZWA NA MAMA MDOGO WA MAREHEMU KUWEKA SHADA LA MAUA KATKA KABURI ALILOLALA ESTER |
MWAKILISHI WA VICTORIA FOUNDATION STEVEN MRUMA BAADA YA KUTOA SHUKRANI ZAKE MARA BAADA YA MAZISHI |
BAADHI YA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WALIOKUJA KUMSINDIKIZA ESTER KATIKA SAFARI YAKE YA MWISHO. |
NA HAPA NDIPO SAFARI YA MWISHO YA DUNUANI YA ESTER ILIPOISHIA BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.. "Ameen" |
No comments:
Post a Comment