Monday, 7 July 2014

PICHA: NI NOMA SANA HAYA NDIYO YALIYOTOKEA JANA KATIKA BIRTHDAY PARTY YA MTOTO WA MH. VICKY KAMATA

Na Steven Mruma

         Jana ilikua ni siku ya kuzaliwa ya mtoto wa Mh. Vicky Kamata na kama kawaida lilianguka booonge la party nyumbani kwa Mh. Vicky Sinza Vatcan.
        Kuacha tukio zima la Birthday party kuna mambo mengi sana yalitokea mengi yalikua ya kufurahisha sana na wakati mwingine hata kushangaza pia, laikin kwa ujumla wake ilikua ni siku tofauti sana kuwahi kutokea nyumbani kw Mh. Vicky Kamata.
    
      MATUKIO YA PEKEE SANA AMBAYO YATAKUJIA MOJA BAADA YA JINGINE ILI UWEZE KUJUA NI NINI HASA KILITOKEA NI KAMA IFUATAVYO:-
  1. Disco la nguvu ambalo watu walicheza vya kutosha ikiwemo Mh. Vicky Kamata ambaye alionyesha uwezo mkubwa sana katika kucheza muziki hasa wa kizazi kipya na katika tukio hilo nitakuletea video pamoja na picha zikiwa tayari
  2. Tukio jingine lilikua la maandalizi kufanyika kwa ustadi mkubwa na kwa haraka hali iliyopelekea mpaka Mh. Vicky kusahau kuvaa viatu mara kwa mara na kujikuta kupiga picha na wageni akiwa hana viatu.
  3. Marafiki wengi sana walijitokeza na wengi walipiga nae picha ya pamoja kama kumbukumbu.. si mara zote unaweza kupata nafasi ya kupiga picha na Mh. Vicky kamata
  4. kulikua na mashindano ya kucheza ambayo yalishirikisha zaidi watoto na hakika watoto walionyesha uwezo mkubwa sana japo umri wao ulikua mdogo sana.
  5. Kwa mara ya kwanza Mh. Vicky kamata ali perform wimbo wake mpya wa Moyo wa mtu kichaka na baada ya shoo hiyo alitamka maneno mazito ambayo ningependa uyafaham..  
  6. Muonekano mpya wa nyumba ya Mh. Vicky Kamata na mambo mengi ya kifamilia na jinsi anavyoishi na familia yake, 
   Hayo yalikua ni baadhi tu ya yaliyotokea jana na kila tukio litakujia kwa namna yake na kwa uchambuzi wa kina.. enedelea kufuatilia VICKY KAMATA BLOG PAMOJA NAMI Steven Mruma International article writer

HIZI NI BAADHI YA PICHA CHACHE ZA BIRTHDAY PARTY HIYO NA MATUKIO MENGI YATAKUJIA MUDA SI MREFU

MOJA KATI YA KEKI ZA BIRTHDAY YA MTOTO WA MH. VICKY
KEKI ZILIZOANDALIWA KWA AJILI YA SHUGHULI NZIMA YA BIRTHDAY PARTY
 

WATOTO WAKIJICHANA KABLA YA HAFLA YA BIRTHDAY KUANZA

WATOTO WAKIFANYA YAO

 

STEVEN MRUMA [KATIKATI] PAMOJA NA WANAKATI YA CHAKULA NA VINYWAJI WINNIE KUSHOTO NA PETER KULIA

BAADHI YA PICHA NA WAGENI WAKATI WA MAANDALIZI NA HII NI MOJA KATI YA PICHA NYINGI MH. VICKY KAMATA
MH. VICKY AKIWAGAWAIA WATOTO WALIOJUMUIKA KATIKA BIRTHDAY PARTY YA MWANAE

HAPA NI MWAZNO TU WA SHEREHE HIYO NA MATUKIO MENGI YA KEKI MUZIKI NK ENDELEA KUFATILIA BLOG HII.
PICHA YA PAMOJA NA WADOGO ZAKE [ KULIA NI MUANDISHI WA HABARI ZA BLOG HII Steven Mruma 'Trust']


3 comments:

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI