Mtaalam wa Mifugo akiwapa chanjo vifaranga.
|
TARATIBU NA RATIBA ZA UCHANJAJI
Wakati
wa kutayarisha mpango wa kuchanja kuku kwa ajili ya kinga dhidi ya
magonjwa, kuna vipengele vikuu sita Ambavyo unatakiwa uvifahamu na
kuvizingatia. Vipengele hivyo ni kama ifuatavyo:
Iwapo una kundi zaidi ya moja la vifaranga wanaoanguliwa,
Weka utaratibu wa chanjo ambao utapunguza uwezekano wa magonjwa kuenea shambani. Hivyo basi,
2. Umri wa kuchanja kuku:
Kwa kuku ambao wanatarajiwa kutaga mayai au kuwa kuku wazazi, chanjo
nyingi
hutolewa si zaidi ya mwezi mmoja kabla ya kuku kuanza kutaga. Pia kuna
baadhi ya chanjo ambazo haziruhusiwi kwa kuku wadogo. (Angalia Ratiba).
3. Magonjwa muhimu katika eneo husika:
Ni
muhimu sana kuelewa magonjwa ya kuku yaliyopo katika eneo lako kabla ya
kuandaa programu ya uchanjaji, hasa kwa yale magonjwa ambayo chanjo
zenye
Ugonjwa huo haujawahi kuripotiwa.
4. Hali ya kiafya ya kuku watakaochanjwa:
Usiwape
chanjo kuku ambao wanaonyesha dalili za kuathirika kwa mfumo wa hewa au
wanaonyesha kuwa na minyoo au wadudu wengine. Kwa kuku walio na dalili
hizi chanjo zinaweza kuleta madhara na zisifanye kazi.
5. Aina ya kuku watakaochanjwa:
Kuku
wanaofugwa kwa ajili ya nyama wanahitaji kinga ya muda mfupi, hivyo
basi chanjo moja inaweza kutosha kabla ya kufikia umri wa kuuzwa. Lakini
kuku wa mayai na kuku wazazi wanahitaji programu ya chanjo ambayo
itawakinga na magonjwa kwa kipindi chote wanapokua na kutaga. (Zingatia
Ratiba).
6. Historia ya Magonjwa katika shamba:
Kabla ya kuandaa mpango wa chanjo, lazima ufahamu ni
Magonjwa gani yaliyoenea katika shamba.
a) Kama unataka kuingiza kuku wapya kutoka mahali ambako ugonjwa umeshawahi kutokea,
kuku hao wachanjwe wiki 3 kabla ya kuwaingiza shambani
b) Iwapo utatumia chanjo yenye vimelea hai, hakikisha kwamba magonjwa hayo yameshawahi
kutokea katika shamba husika. Usitumie chanjo hizi katika shamba ambalo ugonjwa huo
haujawahi kutokea au kutambuliwa.
c) Wasiliana na mashamba jirani kufahamu iwapo wanatumia chanjo zenye vimelea hai. Toa taarifa
kwa mamlaka za mifugo iwapo unapanga kutumia chanjo hizo katika eneo lako. Pata ushauri wa daktari.
TARATIBU ZA UCHANJAJI
Mambo muhimu ya kuzingatia:
•Hakikisha
unazingatia kwa makini masharti ya mtengenezaji wa chanjo: jinsi ya
kuhifadhi, kutayarisha na njia inayotumika kumchanja kuku. Wakati wote
zingatia masharti ya mtengenezaji kuhusu uhifadhi wa chanjo ili isipoteze nguvu.
• Fuata ushauri wa daktari wa mifugo unapoandaa programu ya chanjo.
• Watoa chanjo wapatiwe mafunzo ya jinsi ya kutayarisha na kutoa chanjo
• Chagua aina ya chanjo kulingana na umri na hali ya kiafya ya kuku.
• Fanya usafi wa mara kwa mara katika mabanda ili kupunguza wingi wa vimelea kwenye mazingira.
•
Tumia maji ambayo hayajawekwa dawa au kemikali kwa ajili ya
kuchanganyia chanjo, k.m. maji ya kisima, mvua, n.k. Maji ya
kuchanganyia chanjo yawe na ubaridi, yasiwe moto.
• Changanya chanjo kabla ya kutumia na iwekwe mbali na kuku.
• Pata ushauri wa daktari wa mifugo kabla ya kuchanja kuku wagonjwa au wale ambao hawako katika muonekano mzuri
• Siku ya chanjo, usiwape kuku maji kwa masaa 3 – 4 ili waweze kunywa maji yaliyowekwa chanjo kwa haraka.
• Zoezi la uchanjaji lifanyike haraka ili kupunguza usumbufu kwa kuku.
• Tenganisha kuku waliochanjwa na wale ambao hawajachanjwa.
• Baada ya kuchanjwa, kuku wawekwe kwenye banda linalopitisha hewa vizuri
•
Baada ya kila zoezi la kuchanja, wafanyakazi wabadilishe mavazi,
viatu/buti zisafishwe na kuwekwa dawa, na vifaa vilivyotumika viwekwe
dawa ya kuua vimelea.
• Fuata utaratibu uliowekwa wa kuharibu/kusafisha vifaa vilivyotumika kuchanja
• Weka kumbukumbu za uchanjaji vizuri
Mambo ambayo hutakiwi kuyafanya unapochanja
• Kumwaga chanjo ovyo na kuchafua mikono au nguo
• Kuchanganya chanjo za aina mbili au zaidi, isipokuwa pale tu mtengenezaji wa chanjo atakavyoagiza
hivyo, au kwa ushauri wa daktari wa mifugo.
• Kutumia chanjo iliyopita muda wake
• Kutumia chanjo iliyobaki ili itumike kwa kazi ya siku nyingine
• Kuchanja kuku ambao wamepatiwa dawa aina ya antibiotiki.
• Kuchanja zaidi ya chanjo moja kwa wakati, iwapo haikuagizwa hivyo.
CHANJO ZINAZO PENDEKEZWA
Aina ya Chanjo
|
Umri wa Kuchanja Kuku
|
Muda kati ya kutoa chanjo
|
Njia inayotumika kuchanja kuku
|
Lasota – kwa ajili ya Mdondo/Kideri
|
Kifaranga wa Siku 3
|
Rudia baada ya siku 21, baada ya hapo kila baada ya miezi 3
|
Maji safi yasiyowekwa dawa
|
Chanjo inayohimili joto - I-2 kwa ajili ya Mdondo/Kideri
|
Kifaranga wa Siku moja
|
Rudia baada ya kila miezi 4 kwa kuku wa mayai na wazazi
|
Tone la chanjo kwenye jicho kwa kila kuku
|
Hipraviar-B1 - kwa ajili ya
Mdondo/Kideri na Ugonjwa wa Mapafu (Infectious Bronchitis)
|
Kifaranga wa Siku moja
|
Rudia baada ya siku 21, baada ya hapo kila baada ya miezi 3
|
Maji safi yasiyowekwa dawa
|
VIR-114 – kwa ajili ya Gumboro
|
Siku 10 au 14
|
Inaweza kurudiwa Siku ya 17 kwa
wale waliochanjwa wakiwa na Siku
10; na Siku ya 28 kwa wale waliochanjwa wakiwa na Siku 14
|
Maji safi yasiyowekwa dawa.
|
Avipro – kwa ajili ya Ndui ya Kuku
|
Wiki 7 hadi 14
|
Chanjo moja
|
Chanja katikati ya ngozi
kwa kutumia utando wa ngozi kwenye bawa
|
Chanjo ya Mareksi
|
Kifaranga wa Siku moja
|
Chanjo moja
|
Chanja ndani ya tumbo au chini ya ngozi
|
Mawasiliano ya Mtaalam 0753226538 kwa msaada zaidi.
1 comment:
Useful info. Fortunate me I discovered your website accidentally, and
I am shocked why this coincidence didn't came about in advance!
I bookmarked it.
my blog post: darkrooms (http://bmp3.xaunicom.com)
Post a Comment