Friday 2 April 2021

MAKALA MAALUM KWA WAFUGAJI WA KUKU: ZIFAHAMU TARATIBU NA RATIBA ZA UCHANJAJI WA KUKU KUANZIA VIFARANGA NA KUKU WAKUBWA.


Mtaalam wa Mifugo akiwapa chanjo vifaranga.
TARATIBU NA RATIBA ZA UCHANJAJI
    Wakati wa kutayarisha mpango wa kuchanja kuku kwa ajili ya kinga dhidi ya magonjwa, kuna vipengele vikuu sita Ambavyo unatakiwa uvifahamu na kuvizingatia. Vipengele hivyo ni kama ifuatavyo:
Kuku wakienyeji ni rahisi sana kuwafuga tofauti na wakisasa.
1. Vifaranga vinavyoanguliwa kwa pamoja:
 Iwapo una kundi zaidi ya moja la vifaranga wanaoanguliwa,
Weka utaratibu wa chanjo ambao utapunguza uwezekano wa magonjwa kuenea shambani. Hivyo basi,
Zipo namna nyingi za uchanjaji wa kuku zingine zinahitaji utaalam
Hakikisha vifaranga na kuku wote wanapata chanjo kwa pamoja.
2. Umri wa kuchanja kuku:
Kwa kuku ambao wanatarajiwa kutaga mayai au kuwa kuku wazazi, chanjo
nyingi hutolewa si zaidi ya mwezi mmoja kabla ya kuku kuanza kutaga. Pia kuna baadhi ya chanjo ambazo haziruhusiwi kwa kuku wadogo. (Angalia Ratiba).
3. Magonjwa muhimu katika eneo husika:
Ni muhimu sana kuelewa magonjwa ya kuku yaliyopo katika eneo lako kabla ya kuandaa programu ya uchanjaji, hasa kwa yale magonjwa ambayo chanjo zenye
Vimelea hai hutumika. Hivyo basi, sio busara kuanza kutumia chanjo za aina hii katika maeneo ambayo
Ugonjwa huo haujawahi kuripotiwa.
4. Hali ya kiafya ya kuku watakaochanjwa:
 Usiwape chanjo kuku ambao wanaonyesha dalili za kuathirika kwa mfumo wa hewa au wanaonyesha kuwa na minyoo au wadudu wengine. Kwa kuku walio na dalili hizi chanjo zinaweza kuleta madhara na zisifanye kazi.
5. Aina ya kuku watakaochanjwa:
Kuku wanaofugwa kwa ajili ya nyama wanahitaji kinga ya muda mfupi, hivyo basi chanjo moja inaweza kutosha kabla ya kufikia umri wa kuuzwa. Lakini kuku wa mayai na kuku wazazi wanahitaji programu ya chanjo ambayo itawakinga na magonjwa kwa kipindi chote wanapokua na kutaga. (Zingatia Ratiba).
6. Historia ya Magonjwa katika shamba:
Kabla ya kuandaa mpango wa chanjo, lazima ufahamu ni
Magonjwa gani yaliyoenea katika shamba.
a) Kama unataka kuingiza kuku wapya kutoka mahali ambako ugonjwa umeshawahi kutokea,
kuku hao wachanjwe wiki 3 kabla ya kuwaingiza shambani
b) Iwapo utatumia chanjo yenye vimelea hai, hakikisha kwamba magonjwa hayo yameshawahi
kutokea katika shamba husika. Usitumie chanjo hizi katika shamba ambalo ugonjwa huo
haujawahi kutokea au kutambuliwa.
c) Wasiliana na mashamba jirani kufahamu iwapo wanatumia chanjo zenye vimelea hai. Toa taarifa
kwa mamlaka za mifugo iwapo unapanga kutumia chanjo hizo katika eneo lako. Pata ushauri wa daktari.

TARATIBU ZA UCHANJAJI
Mambo muhimu ya kuzingatia:                                                                                         
  •Hakikisha unazingatia kwa makini masharti ya mtengenezaji wa chanjo: jinsi ya kuhifadhi, kutayarisha na njia inayotumika kumchanja kuku. Wakati wote zingatia masharti ya mtengenezaji kuhusu uhifadhi wa chanjo ili isipoteze nguvu.                                                     
                     
                         
 • Fuata ushauri wa daktari wa mifugo unapoandaa programu ya chanjo.                                         
  • Watoa chanjo wapatiwe mafunzo ya jinsi ya kutayarisha na kutoa chanjo                                     
   • Chagua aina ya chanjo kulingana na umri na hali ya kiafya ya kuku.                                           
   • Fanya usafi wa mara kwa mara katika mabanda ili kupunguza wingi wa vimelea kwenye mazingira.
 • Tumia maji ambayo hayajawekwa dawa au kemikali kwa ajili ya kuchanganyia chanjo, k.m. maji ya kisima, mvua, n.k. Maji ya kuchanganyia chanjo yawe na ubaridi, yasiwe moto.                                   
 • Changanya chanjo kabla ya kutumia na iwekwe mbali na kuku.                               
     • Pata ushauri wa daktari wa mifugo kabla ya kuchanja kuku wagonjwa au wale ambao hawako katika muonekano mzuri
• Siku ya chanjo, usiwape kuku maji kwa masaa 3 – 4 ili waweze kunywa maji yaliyowekwa chanjo kwa haraka.                                                                                                                           
 • Zoezi la uchanjaji lifanyike haraka ili kupunguza usumbufu kwa kuku.                                                
 • Tenganisha kuku waliochanjwa na wale ambao hawajachanjwa.                                          
         • Baada ya kuchanjwa, kuku wawekwe kwenye banda linalopitisha hewa vizuri                                                   
 • Baada ya kila zoezi la kuchanja, wafanyakazi wabadilishe mavazi, viatu/buti zisafishwe na kuwekwa dawa, na vifaa vilivyotumika viwekwe dawa ya kuua vimelea.                                                             
   • Fuata utaratibu uliowekwa wa kuharibu/kusafisha vifaa vilivyotumika kuchanja                                    
   • Weka kumbukumbu za uchanjaji vizuri
Mambo ambayo hutakiwi kuyafanya unapochanja
• Kumwaga chanjo ovyo na kuchafua mikono au nguo
• Kuchanganya chanjo za aina mbili au zaidi, isipokuwa pale tu mtengenezaji wa chanjo atakavyoagiza
hivyo, au kwa ushauri wa daktari wa mifugo.
• Kutumia chanjo iliyopita muda wake
• Kutumia chanjo iliyobaki ili itumike kwa kazi ya siku nyingine
• Kuchanja kuku ambao wamepatiwa dawa aina ya antibiotiki.
• Kuchanja zaidi ya chanjo moja kwa wakati, iwapo haikuagizwa hivyo.
CHANJO ZINAZO PENDEKEZWA
Aina ya Chanjo
Umri wa Kuchanja Kuku
Muda kati ya kutoa chanjo
Njia inayotumika kuchanja kuku
Lasota – kwa ajili ya Mdondo/Kideri
Kifaranga wa Siku 3
Rudia baada ya siku 21, baada ya hapo kila baada ya miezi 3
Maji safi yasiyowekwa dawa
Chanjo inayohimili joto - I-2 kwa ajili ya Mdondo/Kideri
Kifaranga wa Siku moja
Rudia baada ya kila miezi 4 kwa kuku wa mayai na wazazi
Tone la chanjo kwenye jicho kwa kila kuku
Hipraviar-B1 - kwa ajili ya
Mdondo/Kideri na Ugonjwa wa Mapafu (Infectious Bronchitis)
Kifaranga wa Siku moja
Rudia baada ya siku 21, baada ya hapo kila baada ya miezi 3
Maji safi yasiyowekwa dawa
VIR-114 – kwa ajili ya Gumboro
Siku 10 au 14
Inaweza kurudiwa Siku ya 17 kwa
wale waliochanjwa wakiwa na Siku
10; na Siku ya 28 kwa wale waliochanjwa wakiwa na Siku 14
Maji safi yasiyowekwa dawa.
Avipro – kwa ajili ya Ndui ya Kuku
Wiki 7 hadi 14
Chanjo moja
Chanja katikati ya ngozi
kwa kutumia utando wa ngozi kwenye bawa
Chanjo ya Mareksi
Kifaranga wa Siku moja
Chanjo moja
Chanja ndani ya tumbo au chini ya ngozi
   Mawasiliano ya Mtaalam 0753226538 kwa msaada zaidi.

1 comment:

Anonymous said...

Useful info. Fortunate me I discovered your website accidentally, and
I am shocked why this coincidence didn't came about in advance!

I bookmarked it.

my blog post: darkrooms (http://bmp3.xaunicom.com)

GEITA DOCUMENTARY

Contributors