Thursday 15 November 2012

MIZENGO PINDA KUONGOZA SEMINA KWA MA-RC, DC



WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, leo anarajiwa kuongoza warsha ya uhamasishaji kuhusu majadiliano ya ushirikiano kwa manufaa ya wote (Smart Partnership Dialogue) kwa wakuu wote wa mikoa (ma-RC), makatibu tawala na wakuu wa wilaya (ma-DC) zote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Samson Chemponda, alisema maandalizi ya warsha hiyo yamekamilika na itatoa uelewa mkubwa kuhusu majadiliano ya kitaifa yatakayofanyika Januari mwakani.
“Hii ni warsha muhimu, kwani itachochea kasi ya uhamasishaji wa majadiliano hayo kabla ya majadiliano ya kitaifa hapo Januari na yale ya kimataifa hapo Mei mwakani,” alisema Chemponda.
Kwa mujibu wa mtendaji huyo, warsha hiyo ya wakuu wa mikoa, makatibu tawala na wakuu wa wilaya itahamasisha kuhusu umuhimu wa midahalo ya aina hiyo kutoka ngazi ya wilaya na hatimaye mkoa kupitia mabaraza ya biashara ya mikoa (RBCs) na ya wilaya DBCs.
Mchakato wa majadiliano ulishazinduliwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Mei 29, mwaka huu.
Alisema majadiliano hayo yatasaidia kupata mawazo na mbinu mbali mbali za kuibua vipaji vya vijana na kuvilinda, ili kuleta msukumo wa kuimarisha masuala ya sayansi na teknolojia.
Kaulimbiu ya majadiliano hayo ni ‘Leveraging Technology for Africa’s Socio-Economic Transfomation: The Smart Partnership Way’ ambayo inalenga kuleta mapinduzi ya uchumi kupitia teknolojia na kutoa msukumo wa utekelezaji wa sera mbalimbali kama vile Kilimo Kwanza, MKUKUTA, MKUZA, MKURABITA na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

1 comment:

Anonymous said...

Its like you read my mind! You seem to know a lot about this, like you wrote the book in it or something.

I think that you can do with a few pics to drive the message home a little bit,
but other than that, this is wonderful blog. A great read.
I'll definitely be back.
My web page - Do Not Click Here

GEITA DOCUMENTARY

Contributors