Wednesday 14 November 2012

KIKWETE MWENYEKITI TENA CCM, MANGULA, DK, SHEIN MAKAMU WAKE

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Makamu wenyeviti wawili, Spika wa Bunge Anna Makinda, baada ya kumtangaza kushinda nafasi hiyo ya Uenyekiti, katika uchaguzi uliofanyika jana katika ukumbi wa Kizota, Dodoma, ikiwa ni kuhitimisha shughuli za Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM. Wapili Kulia ni Makamu Mwenyekiti Mpya wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal
 Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Jakaya Kikwete na Makamu wake wawili Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (Zanzibar) na Philip Mangula (Bara) wakiwa meza kuu baada ya kutangazwa kushika nyandhifa zao.
 Wajumbe wakiserebuka baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangazwa kuwa mshindi wa Uenyekiti wa CCM, Taifa.
 Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete akiongoza kikao baada ya kushinda tena kiti hicho. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Sheni na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Phili Mangula. 

                            PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
                                   www.ccmchama.blogspot.com 

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors