Wednesday 21 November 2012

ASKARI WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA



HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa askari wawili wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mmoja wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kumuua kwa kusudia, Swetu Fundikira.
Askari hao MT 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa JKT, Kikosi cha Mbweni, MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ, Kikosi cha Kunduchi na MT 85067 Koplo Mohamed Rashid wa JKT Mbweni.

Washitakiwa hao walidaiwa kumpiga na hatimaye kumuua kwa makusudi Fundira Januari 23, majira ya saa 7:30 usiku wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam na kufariki dunia usiku wa kuamkia Januari 24 mwaka 2010, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.

Sweti Fundikira ni mtoto wa mdogo wa Mwanasiasa Maarufu nchini, marehemu Chifu Abdallah Fundikira.
Hukumu hiyo ambayo inaweza kukomesha vitendo vya askari kujichukulia sheria mkononi dhidi ya raia, ilitolewa jana na Jaji Zainabu Muruke.

Jaji Muruke alisema baada ya kusikiliza kesi hiyo, ameridhika na ushahidi uliotolewa na mawakili wa upande wa Serikali ambao ulidai kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo la mauji kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.

Akisoma hukumu hiyo iliyovuta hisia za wengi mahakamani hapo, Jaji Muruke alisema ingawa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonesha washtakiwa hao kuwa ndiyo waliomua marehemu (Fundikira), ushahidi mazingira unaonesha pasipo shaka walihusika na mauaji hayo.

“Sheria ipo wazi na inaanisha kuwa ukiondoka au ukionekana na mtu kwa mara ya mwisho na baadaye mtu huyo uliyeondoka naye akapata madhara au amekutwa amekufa, wewe uliyeondoka naye ndiyo utawajibika kisheria na madhara yaliyompata mtu huyo;

“Japo kuwa ushahidi uliotumiwa na upande wa mashitaka katika kesi hii ni wa mazingira, lakini umeweza kuthibitisha kesi yao, upande wa utetezi nao umeweza kutoa ushahidi wenye matundu mengi na unaokatika katika sana na ambao umeshindwa kuudhoofisha ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri dhidi ya washtakiwa, ’alisema jaji Mruke.
Aidha, alisema Jamhuri imeweza kuthibitisha kosa la mauaji, hivyo mahakama imewaona washtakiwa wote wana hatia ya kumuua Swetu Fundikira.

Hata hivyo, Jaji Muruke kabla ya kutoa adhabu hiyo alimpa nafasi wakili Karoli Muluge pamoja na washtakiwa kusema lolote kabla ya kuwapatia adhabu hiyo.

Wakili Muluge aliiomba Mahakama iwape adhabu ndogo kutokana na mazingira ya kesi hiyo, umri wa washtakiwa kwani bado ni vijana, nguvu kazi ya taifa na familia zao zinawategemea.

Naye mshtakiwa wa kwanza, Sajenti Robert aliiomba Mahakama impunguzie adhabu akidai kuwa mama yake ni mjane na anamtegemea, pia ana watoto wadogo.

Hata hivyo Jaji Muruke alilamuamuru mshtakiwa wa pili, Koplo Ngumbe kukaa chini baada kuanza kujitetea kuwa ametiwa hatiani kimakosa na anamwachia Mungu.

Kwa upande wake mshtakiwa wa tatu, Koplo Rashid aliiomba mahakama imuonee huruma na impunguzie adhabu akidai kuwa bado ni mdogo na hilo ni kosa lake la kwanza.

Akitoa adhabu, Jaji Muruke alisema ni kweli maombi ya mshtakiwa wa kwanza yanatia huruma na kwamba mshtakiwa wa tatu hata kumbukumbu zinaonesha bado ni mdogo, pia hilo ni kosa lake la kwanza, lakini alisema kuna roho iliyopotea.

“Sheria ipo wazi kabisa mshtakiwa yoyote anayepatikana na hatia adhabu yake ni moja tu ambayo ni kunyongwa hadi kufa na hakuna mbadala wa adhabu hiyo…hivyo mahakama hii kwa kauli moja inatamka kuwa washitakiwa wote wa tatu mahakama hii imewahukumu adhabu ya kifo hivyo, mtanyongwa hadi kufa,” alisema Jaji Muruke:

Baada ya kutoa adhabu hiyo Jaji Muruke alitoka katika chumba cha mahakama na ghafla ndugu wa marehemu Fundikira waliangua vilio ndani ya ukumbi wa mahakama, kama vile walikuwa msibani.

Ndugu wawili wa marehemu, Mwasiti Fundikira ambaye ni Dada wa marehemu na Shelina Hamisi (mpwa wa marehemu) walianguka chini na kuzirai kwa muda hali iliyowalazimu watumishi wa mahakama kuwapatia huduma ya kwanza kwa kuwapepea hadi waliporejea katika hali ya kawaida.

Mke wa marehemu, aliyejitambulisha kwa jina la Lucy ambaye aliachwa akiwa mjamzito, alisema hakuamini kama haki ingetendeka kwani mpendwa wao aliuwawa kinyama.
Hata hivyo wakili wa washitakiwa hao, Muluge alisema hakuridhika na hukumu hiyo na kwamba atakata rufaa.

1 comment:

Anonymous said...

Aauzcsywk [url=http://headachetreatment.net/fioricet_faq.html]fioricet info[/url] butalbita, Roaqdfxfi rgc [url=http://relievepain.info/tramadol_precautions.html]tramadol without prescription[/url] tramadol faq, Gyvaqrwyl
CxxTsfroo [url=http://genericviagra.name/partners/]generic viagra[/url] .. buy generic viagra, WqmyjegEwk - [url=http://compracialis.it/articoli/archive/2012/11/17/incapacita-e-astenia-sessuale-una-notizia-cura-disadvantage-le-d]compracialis viagra[/url] .. cialis online; SauujwkRsf

GEITA DOCUMENTARY

Contributors