Friday 19 October 2012

WALEMAVU WENGI HAWAJUI KUSOMA, KUANDIKA



ZAIDI ya asilimia 90 walemavu wa viungo wilayani Karagwe hawajui kusoma na kuandika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kunyanyapaliwa katika jamii.
Hayo yalibainishwa jana mjini hapa na Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu (CHAWATA) wilayani hapa, Hashimu Muhamud, alipozungumza na waandishi.

“Ulikuwa unakuta mtoto mwenye ulemavu alipokuwa akipelekwa shule watoto wenzake wanamcheka na kumzomea na matokeo yake anaamua kuacha shule,” alisema Muhamud.
Alisema baadhi ya walezi na wazazi nao walichangia hali hiyo kutokana na uelewa mdogo wa kuwaficha majumbani watoto hao na kushindwa kuwaandikisha shuleni.

Alisema sababu nyingine inayochangia hali hiyo ni mila potofu kwa baadhi ya familia za kutowatambua watoto wenye ulemavu kuwa sawa na watu wasio na ulemavu.
Kwa upande wake, Katibu wa Chawata Wilaya ya Misenyi, Celestine Mkandara, alisema hali hiyo imechangiwa na miundombinu ya majengo mengi ya mashule kutokuwa rafiki kwa walemavu, hivyo wazazi wengi kushindwa kuwapeleka watoto wao.



 Kwa hisani ya Tanzania Daima

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors