Saturday, 7 April 2012

REST IN PEACE STEVEN KANUMBA 'The Great'



Muigizaji maarufu wa filamu za kibongo Steven Kanumba A.K.A Kanumba The Greit amefariki dunia usiku wa manane kuamkia leo, na maiti iko muhimbili. kwa taarifa zilizopo ni kuwa msiba upo Sinza maeneo ya Vatican, ukifika Vatican Hotel umefika msibani. sababu za kifo chake hazijathibitishwa. stay with us kwa habari zaidi.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI. AMEN


Jina la kuzaliwaSteven Charles Kanumba
Alizaliwa8 Januari 1984ShinyangaTanzania
Kafariki6 Aprili 2012Dar es SalaamTanzania
Kazi yakeMuigizajiMtunziMtayarishajiMuongozaji

MAISHA
Na ameanza elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja ya jiji Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee

Shughuli za uigizaji

Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90". Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.
Kwa sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar to LagosShe is My Sister na nyingine ambazo bado zinajengwa.Hivi sasa amejibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu.

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors