Sunday, 30 May 2010

Wanaotembea na wajawazito watahadharishwa

LONDON,Uingereza

WATAFITI wa masuala ya afya wamesema kuwa wanaume wanakuwa hatarini mara mbili zaidi kuambukizwa virusi vinavyoeneza ugonjwa wa UKIMWI pindi wapenzi wao wanapokuwa wajawazito.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa zaidi ya wanandoa 3,000 barani Afrika na kuungwa mkono na tafiti kadhaa, inaonyesha kuwa wanawake ni rahisi kusambaza virusi hivyo vya UKIMWI pindi wanapokuwa wajawazito.

Watafiti hao wanasema kwamba mabadiliko katika mwili wa mwanamke anapokuwa mjamzito yanachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la nafasi kwa mpenzi wake kuathirika.

Kwa mujibu wa watafiti hao kutoka Uingereza findings, imeoneka kuwepo kwa ulazima wa kupima.

Matokeo ya utafiti huo yatolewa juzi wakati wa mkutano mkuu wa kimataifa wa kumpambana na ugonjwa wa UKIMWI unaofanyika mjini Pittsburgh ambapo sambamba na utafiti huo,tafiti nyingine zimeonesha kuwa njia ya kutumia dawa ya kupaka aina ya microbicidal gel ambayo inaua bakteria ni njia salama kwa wajawazito kujikinga na usambazaji wa virusi vya UKIMWI.

Katika mkutano huo ilielezwa kwamba pia wasichana wenye umri mdogo ni miongoni mwa waliopo hatarini kuambukizwa virusi hivyo vya UKIMWI katika nchi ambazo zina kiwango cha hali ya juu cha ugonjwa huo.

Utafiti huu ni wa kwanza kuonesha kuwa mwanamume ndiye yupo hatarini zaidi kukumbwa na maradhi hayo wakati mkewe anapokuwa mjamzito baada ya tafiti za awali kuonesha mwanamke ndiye alikuwa hatarini zaidi kuambukizwa virusi vya UKIMWI kutoka kwa mpenzi wake wakati wa ujauzito.

Utafiti huo ambao ulifanyika katika nchi za Botswana, Kenya, Rwanda, Afrika Kusini , Tanzania, Uganda na Zambia,uliwahusisha wanandoa 3,321 na mmoja kati yao kuonekana ameathirika huku waliosalia wakiwa hawana virusi hivyo.

Katika kipindi cha miaka zaidi ya miwili ilionesha kuwa kumekuwepo na mimba 823 na uchunguzi unaonesha kwamba maambukizi yameongezeka pande zote kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanamume na kutoka kwa mwanamume kwenda kwa mwanake.

"Changamoto moja kubwa inayotukabili nchini Uingereza ni kwamba mmoja kati ya watu wanne wenye UKIMWI hafahamu kama ana virusi kwa sababu hajapima,"alisema Bw.Jason Warriner,kutoka mfuko wa Terrence Higgins.

Alisema kuwa kwa upande wa wanawake inaonekana wanawake ambao siyo wajawazito ndiyo wanaochangia zaidi kusambaza virusi kuliko wanawake wajawazito lakini akasema kuwa kwa wanaume wenye mahusiano na wanawake wajawazito hawako hatarini sana labda wajihusishe na masuala mengine ikiwemo kufanya ngono isiyo salama.(BBC)

1 comment:

eriq mwidunda said...
This comment has been removed by a blog administrator.

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI