Monday, 26 April 2010

BEAUTY TIPS.!!


Beauty Tips: Jinsi ya kuupa uso wako muonekano wa ngozi tight, laini na ya kuvutia. Siku ya leo beauty tips, tuna njia tatu nyepesi ambazo matokeo yake uonekana baada tu ya kutumia.Ok basi kama uko nyumbani ni vyema ukasogea jikoni kabisa ili kujiandaa kuupa uso wako ngozi changa na yenye afya kwa kipindi kifupi. Mask ya asali: Hii mask ni nzuri sana kwasababu inamoisturizering ngozi yako na ubana vishimo vya ngozi vilivyo wazi.Pia ni nzuri kwa ngozi aina zote. (za mafuta, kavu, na zilizo za wastani). Ingredients: Asali kiasi chochote cha kukutosheleza.
Jinsi ya kutumia: Paka asali kwenye sura yako hadi shingoni kama ukitaka kulinganisha uwastani wa ngozi, lakini kuwa mwangalifu isiingie machoni kwa hiyo ni vyema ukakwepa sehemu za macho.Iache kwa dakika 15 – 30,(relax), kisha osha kwa maji ya vugu vugu. Halafu malizia kuosha na maji ya baridi ili kuziba vishimo vya ngozi zilizokuwa moisturized na asali.Hii ni kwa mtu yeyote, iwe mwanamke au mwanaume wote waweza kutumia hii moisturized asilia kujipa muonekano wa'kichanga(kiupya).

2 comments:

TINAH said...
This comment has been removed by a blog administrator.
MAULID said...
This comment has been removed by a blog administrator.

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI