Tuesday, 10 April 2012
RATIBA RASMI YA MAZISHI YA STEVEN KANUMBA LEO
Msanii wa filamu, aliyebeba mapenzi makubwa ya Watanzania, Waafrika na dunia kwa jumla, Steven Charles Kanumba aliyefikwa na mauti ghafla Aprili 7, 2012, atazikwa kesho Makaburi ya Kinondoni, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Mazishi ya Kanumba, yamepangwa na kuratibiwa kwa kuzingatia heshima, umaarufu, mapenzi yake kwa watu na hadhi ya kimataifa aliyonayo, hivyo imetolewa fursa ya wengi kumuaga msanii huyo ambaye ni mwanamapinduzi wa tasnia ya filamu ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati.
Mpangilio wa ratiba na nafasi itatolewa kwa kila mtu mwenye kuhitaji kushiriki mazishi ya Kanumba, kufanya hivyo katika tukio la kihistoria la kumsindikiza ndugu yetu huyo kwenye maisha ya milele. Hivyo, wito unatolewa kwa kila mtu kujitokeza kwenye shughuli nzima.
RATIBA
Mwili wa marehemu Steven Kanumba utachukuliwa kwa msafara kutoka Hospitali ya Taifa, Muhimbili saa 2:30 asubuhi. Utapitishwa Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambako Misa ya kumuombea itasomwa pamoja na salamu mbalimbali kabla ya watu wote kumuaga.
Wito unatolewa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuanzia saa 2:00 asubuhi, wakijipanga kando ya Barabara za Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi ili wautolee heshima mwili wa Kanumba wakati ukitolewa Muhimbili kwenda Leaders Club.
Saa 3:30 asubuhi, mwili wa Kanumba utapokelewa Viwanja vya Leaders, ukitanguliwa na mapokezi ya wazazi wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao kabisa atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Saa 4:00, itakuwa ni muda wa kusoma Misa ambayo itachukua dakika 60, saa 5:00 kitakuwa kipindi cha salamu kutoka kwa watu mbalimbali.
Saa 6:00 mchana, ratiba ya kumuaga Kanumba itaanza mpaka saa 9:00 alasiri na baada ya hapo, utakuwa wakati wa kuusafirisha mwili kwa msafara kutoka Leaders Club mpaka Makaburi ya Kinondoni, msafara ukipita Barabara ya Tunisia, utakatisha Barabara ya Kinondoni kuelekea makaburini.
Saa 10:00 alasiri, mazishi yatafanyika kwa kufuata utaratibu wa imani ya marehemu.
Kamati ya Mazishi inatoa wito kwa watu watakaohudhuria shughuli ya kumzika ndugu yetu Kanumba, kuja na maua ili kumuaga kwa heshima.
Utulivu, unyenyekevu na ustahimilivu ni mambo muhimu yanayohitajika katika kipindi chote cha kumuaga mpendwa wetu Kanumba.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Sisi wote tulimpenda kwa dhati na tulitamani aendelee kuwa nasi siku zote ila Mungu aliyemleta kwa mapenzi yake ameamua kumchukua. Jina lake lihimidiwe.
K.N.Y GABRIEL MTITU
MWENYEKITI WA KAMATI YA MAZISHI
MADAKTARI WAELEZA KILICHOMUUA KANUMBA
Msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitaalamu kama BRAIN CONCUSSION, taarifa za kitabibu zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani, zimepatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa hospitali ya taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehem, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.Mmoja wa madaktari hao ambae aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya masaa mawili.
"tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu Brain Concussion" alisema. Kanumba alipata mtikisko huo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) "kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehem ya nyuma ua ubongo (cerebram), huua kwa haraka" alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma husababusha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
"Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji unafeli na ndio maana tumekuta kucha za kanumba zikiwa na rangi ya blue, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ni dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji"
"Mtu aliepata mtikisko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.
Daktari mwingine alieshiriki katika uchunguzi huo ambae pia aliomba jina lake lisitahwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji. Alisema sehemu ya maini na maji maji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo
Saturday, 7 April 2012
CHANZO CHA KIFO CHA KANUMBA HIKI HAPA
KWA MUJIBU WA MDOGO WA MAREHEMU STEVE KANUMBA, ALISEMA KUWA ELIZABETH MICHAEL MAARUFU KAMA LULU ALIKUJA NYUMBANI KUKAWA NA KAUGOMVI AMBAPO WAKAINGIA CHUMMBANI WAKIWA HUKO BAADA YA MUDA,LULU ALITOKA NA KUMUITA YEYE KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA, YE ALIPOENDA AKAMKUTA KAANGUKA NDIO AKAENDA MUITA DAKTARI WA KANUMBA AMBAPO ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU, LAKINI HADI TUNAVYOONGEA LULU YUKO POLISI OSTERBAY KWA AJILI YA MAHOJIANO NA POLISI
HAPPY EASTER WISHES TO ALL..
Easter bring Fun, Easter bring Happiness,
Easter bring God Endless Blessings,
Easter bring fresh love…
Happy Easter to You
with all best wishes
Easter bring God Endless Blessings,
Easter bring fresh love…
Happy Easter to You
with all best wishes
REST IN PEACE STEVEN KANUMBA 'The Great'
Muigizaji maarufu wa filamu za kibongo Steven Kanumba A.K.A Kanumba The Greit amefariki dunia usiku wa manane kuamkia leo, na maiti iko muhimbili. kwa taarifa zilizopo ni kuwa msiba upo Sinza maeneo ya Vatican, ukifika Vatican Hotel umefika msibani. sababu za kifo chake hazijathibitishwa. stay with us kwa habari zaidi.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI. AMEN
| Jina la kuzaliwa | Steven Charles Kanumba |
| Alizaliwa | 8 Januari 1984, Shinyanga, Tanzania |
| Kafariki | 6 Aprili 2012, Dar es Salaam, Tanzania |
| Kazi yake | Muigizaji, Mtunzi, Mtayarishaji, Muongozaji |
MAISHA
Na ameanza elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja ya jiji Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee
Shughuli za uigizaji
Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90". Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.
Kwa sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar to Lagos, She is My Sister na nyingine ambazo bado zinajengwa.Hivi sasa amejibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu.
Friday, 23 March 2012
Marekebisho ya Anuani ya Victoria Foundation
Yaliyofanyika katika graphic iliyotumika kwenye blog ya Issa Michuzi
Kutoa shukrani kwa Wafadhili wa Victoria Foundation tarehe 22.03.2012
Katika graphic hiyo inaelekeza kimakosa kuwa ofisi zetu zipo Uhuru Street
Mnazi Mmoja.Taarifa sahihi ni kwamba ofisi zetu zipo Nkrumah Street,
LIDA HOUSE, 2nd Floor.
"TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE ULIOJITOKEZA"
Subscribe to:
Posts (Atom)





