Wednesday, 27 February 2013

TIB, SIDO kujenga maeneo ya viwanda

BENKI ya Rasilimali Tanzania (TIB) imesaini makubaliano na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo nchini (SIDO) yenye lengo la kushirikiana kuweka miundombinu ya viwanda kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo. Mpango huo utawezesha ujenzi wa maeneo ya viwanda ambao utaanza na mkoa wa Dar es Salaam, kabla ya kutanuka katika miji mingine. Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo jijini katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Peter Noni, alisema lengo ni kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa za viwandani. “Hapa benki tumebaini kwamba kuna matatizo makubwa kwa mjasiriamali Mtanzania anapojaribu kuwekeza kwa ajili ya uzalishaji. Vita vya kuondoa umaskini nchini vinategemea uzalishaji. Uzalishaji pia unategemea uwezo wa kupata mikopo kutoka benki. “Huu utaratibu pia utamwezesha mjasiriamali kukopesheka na taasisi za kibenki, kwa sabau atakuwa na mahala maalumu pa kuzalishia kwa gharama ndogo,” alisema Noni. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Michael Laizer, alisema riba ya mikopo inayotolewa na benki nchini bado ni changamoto kwa wajasiriamali wadogo kwa sababu ni kubwa mno. “Riba hizo zinawakwamisha wajasiriamali, zinawarudisha nyuma na pia wanashindwa kupanua biashara zao,” alisema Laizer. Alisema ushirikiano wa SIDO na TIB utawasaidia wajasiriamali watakaoingia katika mpango huo kupata maeneo ya kuanza uzalishaji kwa gharama nafuu.

No comments:

Inspirational Prayer of the Day

choose your favorite language

GEITA DOCUMENTARY

HABARI NYINGINE ZAIDI