Msanii wa Kundi la Vichekesho, Mkwere kutoka kundi la Mizengwe akiigiza kama Askari wa Usalama wa Barabarani akisimamisha magari wakati wakitoa burudani katika Uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa leo mjini Iringa katika Uwanja wa Samora. Maadhimisho hayo yameanza leo Septemba 17-22, 2012. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA"
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani. Dk. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed Jabri Sasi, baada ya Waziri kuwsili uwanja wa Samora Iringa.
Waziri Nchimbi akisalaimMbunge wa Viti Maalum, Rita Moto Kabati na viongozi wengine wa Mkoa wa Iringa
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la SUMATRA katika uwanja wa Samora. Wanaoshuhudia katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Ahmad Kilima, na Meneja Uhusiniano, David Mzirai.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalkama Barabarani, Mohamed Mpinga, ambaye pia ni Katiraza la Usalama Barabarani, akizungumza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma akizungumza
Mtaalam wa Kughani utenzi, Mpemba Asilia akiwajibika
Meza Kuu, Mgeni Rasmi, Waziri wa Mambo ya ndani, Dk.Emmauel Nchimbi (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabani Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed Jabri wakipokea maandamano.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, pamoja na viongozi wengine wakimsikilizo Meneja Mauzo na Masoko wa Makampuni ya ASAS ya Mjini Iringa, Ahmed Omar Kassu juu ya bidhaa mbalimbali za maziwa wanazozalisha na ubora wake Afrika Mashariki, Wakati Waziri alipotembelea banda la ASAS lililopo katika maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Iringa leo.
Mkaguzi Msaidizi wa Kikosi cha Polisi zima Moto na Uokoaji, Elia Kakwembe akitoa maelezo ya namna kusajili makampuni binafsi ya Zimamoto na uokoaji kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.
Mkaguzi wa Polisi, Abel Swai Kutoka Trafiki Makao Makuu jijini Dar es Salaam akitoa maelezo ya namna ajali za barabarani zinaweza kuepukika endapo watumiaji wa barabara watakuwa waangalifu na kufuata sheria za barabarani. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.
Kaimu Mkurugenzi wa SUMATRA, Ahmed Kilima akipokea cheti cha heshima kutoka kwa Waziri wa Mambo ya ndani.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya ASAS, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed, akipokea cheti cha heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, akimkabidhi cheti cha heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda.Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.
Wanafunzi wakipatiwa maelezo ya matumizi yaa yasiyo sababisha ajali.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (kushoto) akimkabidhi Moderm ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadha,mini wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa inayofanyika mkoani Iringa. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani. Pereira Silima (wapili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yameanza leo kitaifa Mkoani Iringa.
Wanafunzi wa shule mbalimbali za Mkoani Iringa wakiimba nyimbo za kuhamasisha jamii kufuata sheria watumibara kuepusha ajali.
Kiongozi wa Kundi la Wazee Sugu, King Kikii, akiongeza waimbaji wa kundi hilo kutoa burudani ya muziki katika uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa iliyoanza jana mkoani Iringa.
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia maadhimisho hayo.
Bendi ya Polisi Jazz kutoka Dar es salaam ilitumbuiza.
Baadhi ya walemavu wakiingia uwanjani katika uwanja wa Samora mjini Iringa katika Uzinduzi wa Wiki ya kitaifa ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa jana mjini hapa huku Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel ikiwa mdhamini mkuu.
No comments:
Post a Comment