Tuesday, 7 January 2014

HALI YA AFYA YA MTOTO JEREMIA ANAYELELEWA NA VICTORIA FOUNDATION INAZIDI KUIMARIKA "TUZIDI KUMUOMBEA".

Na Steven Mruma..

    Hali ya mtoto Jeremia anayelelewa na VICTORIA FOUNDATION inazidi kumarika baada ya madaktari kuufanyia uchunguzi mguu wake walioufanyia upasuaji wa kuweka vyuma mguuni miezi michache iliyopita, kuonyesha hali ya matumaini ya kupona. Akizungumza kwa furaha Jeremia aliomba watanzania wazidi kumuombea hali yake iimarike zaidi kwani inachangia kumrudisha nyumba kimasomo.
    Lakini kwasasa Jeremia anafurahia hali hiyo baada ya mguu wake huo kumsumbua kwa miaka kadhaa sasa bila matumaini ya kupona, Lakini Leo madaktari wamedhibitisha kuwa hali yake inaendelea vizuri na kuna matumaini makubwa sana ya kupona. Jeremia ni Moja kati ya watoto wanofadhiliwa [kulelewa] na Victoria Foundation.
M/kiti wa Victoria Foundation Mh. Vicky Kamata [kushoto] Jeremia [katikati] na Dr. Fulvio Franceschi ambaye ni MD. Orthipaedic Surgeon hospitali ya CCBRT

Jeremia [kushoto] na Dr. Fulvio Franceschi ambaye ni MD. Orthipaedic Surgeon hospitali ya CCBRT
Dr. Fulvio Franceschi ambaye ni MD. Orthipaedic Surgeon hospitali ya CCBRT, Jeremia na Dada Maria aliyemfanyia dressing Jeremia wakati alipokuwa Hospitali CCBRT.

Dada Maria aKImfanyia dressing Jeremia wakati alipokuwa Hospitali CCBRT.
Dr. Fulvio Franceschi ambaye ni MD. Orthipaedic Surgeon hospitali ya CCBRT Akichunguza kwa makini mguu wa mtoto  Jeremia.

Dr. David wa CCBRT Akiufanyia  X-Ray mguu wa Jeremia
Picha ya X-Ray ikiuonyesha mguu ulivyo sasa kwa ndani...

HAPPY BIRTHDAY MWIGULU NCHEMBA MPIGANIA HAKI ZA WANYONGE..


    Leo ni siku ya kuzaliwa mbunge wa Iramba Mwigulu Chemba ambaye pia ni Naibu katibu mkuu wa CCM. Vicky Kamata blog inamtakia maisha marefu na mafanikio mema katika ujenzi wa Taifa la Tanzania.. 

NA HAYA NI MANENO YA SHUKRANI YA MWIGULU NCHEMBA KWA WALIOMTUMIA SALAM ZA SIKU YA KUZALIWA.
     " Napenda Kuwashukuru Wote Mlionitumia Salamu za Siku ya Kuzaliwa Kwangu.Nimefarijika sana,nimetambua Salamu Za Kila mmoja wenu,Kujibu ni nyingi mno(Zaidi ya Elfu 5).Kwa Umoja wenu nasema "ASANTENI SANA,UMOJA NI USHINDI" tuendelee kushirikiana,kukosoana kwa hoja,Urafiki wa Amani na Upendo Udumu Daima."
Mh. Mwigulu Nchemba..

    CV YA MH. MWIGULU LAMECK NCHEMBA KWA UFUPI.

GENERAL
Salutation Honourable Member picture
First Name: Mwigulu
Middle Name: Lameck
Last Name: Nchemba
Member Type: Constituency Member
Constituent: Iramba Magharibi
Political Party: CCM
Office Location: Box 52 Kiomboi, Iramba
Office Phone: +255 878 513446/+255 757 946223
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: mnchemba@parliament .go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 7 January 1975
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of Dar Es Salaam Masters(Economics) 2004 2006 MASTERS DEGREE
University of Dar Es Salaam Degree (Economics) 2001 2004 GRADUATE
The East African Uongozi Institute Management 2002 2003 CERTIFICATE
Mazengo Secondary School A-Level Education 1998 2000 HIGH SCHOOL
Ilboru Secondary School O-Level Education 1994 1997 SECONDARY
Makunda Primary School Primary Education 1987 1993 PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
The Parliament of Tanzania Member - Iramba West Constituency 2010 2015
The Bank of Tanzania Economist I 2006 2010
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - UVCCM National Meeting 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - National Executive Committee (NEC) 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - District Youth Board 2001

Thursday, 2 January 2014

TANZIA. WAZIRI WA FEDHA DR W. MGIMWA AFARIKI DUNIA NCHINI AFRIKA KUSINI...SOMA RATIBA YA MAZISHI NA HISTORIA YAKE KWA UFUPI.





        WAZIRI WA FEDHA MHE. DKT. WILLIAM A. MGIMWA (MB.) ALIFARIKI DUNIA JANA KIFO HICHO KILICHOTOKEA TAREHE 01 JANUARI, 2014 HUKO AFRIKA KUSINI, KATIKA HOSPITALI YA  KLOOF MEDI-CLINIC, PRETORIA. MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIWA KUWASILI SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 04/01/2014NA UTASAFIRISHWA KWENDA MKOANI IRINGA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 05/01/2014 KWA MAZISHI
        IBADA NA TARATIBU ZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU ZITAFANYIKA UKUMBI WA KARIMJEE TAREHE 05/01/2014 KUANZIA SAA 5.30 ASUBUHI.
      MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN..

HISTORIA fupi ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Dr. William Mgimwa aliyefariki dunia nchini Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Kuzaliwa: Januari 20, 1950 Kalenga Iringa.

Elimu:
1966 - 1967 Shule ya Msingi Tosa

1961 -1965 Shule ya Msingi Wasa

1970-1971 Seminari ya Mafinga

1968 - 1969 Tosamaganga Sekondari

1975 - 1984 Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) - Postgraduate in Finance

1989 - 1991 IDM Mzumbe (MBA - Finance)


Ajira
1981 - 2000 - NBC Ltd (Mhasibu, Mhadhiri, Mkurugenzi, Mkurugenzi Mkuu)

2000 - 2010 - Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania Mwanza (Mkuu wa Chuo)

2010 - 2013 - Mbunge, Kalenga (CCM).


 

Member of Parliament CV

GENERAL
Salutation Honourable Member picture
First Name: William
Middle Name: Augustao
Last Name: Mgimwa
Member Type: Constituency Member
Constituent: Kalenga
Political Party: CCM
Office Location: Box 80373, Dar Es Salaam
Office Phone: +255 754 765644/+255 684 765644
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: wmgimwa@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 20 January 1950
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Institute of Development Management, IDM, Mzumbe MBA (Finance) 1989 1991 MASTERS DEGREE
Institute of Finance Management, IFM Postgraduate (Finance) 1983 1984 POSTGRADUATE
Institute of Finance Management, IFM Advanced Diploma (Banking) 1975 1978 ADV DIPLOMA
Tosamaganga Seminary School O-Level Education 1968 1969 SECONDARY
Mafinga Seminary School O-Level Education 1970 1971 SECONDARY
Wasa Primary School Primary Education 1961 1965 PRIMARY
Tosa Seminary Primary School Primary Education 1966 1967 PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
The Parliament of Tanzania Member - Kalenga Constituency 2010 2015
Bank of Tanzania Training Institute (Mwanza) Principal 2000 2010
The National Bank of Commerce (NBC) - Bank Director 1997 2000
The National Bank of Commerce (NBC) - Bank Manager 1996 1997
The National Bank of Commerce (NBC) - College Lecturer 1981 1989
The National Bank of Commerce (NBC) - Bank Accountant 1980 1981
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi, CCM Ward Guardian (Wasa, Iringa) 2008 2010
Chama Cha Mapinduzi, CCM Assistant Commander (UVCCM) 1994 1995
Chama Cha Mapinduzi, CCM Councillor (Gangilonga Ward) 1991 1994
PUBLICATIONS
Description Date
W. Mgimwa: Liquidity Management, Tanzania Bankers Journal, Dar Es Salaam. 1994
W. Mgimwa: Commercial Bank Lending Journal, Dar Es Salaam. 1995
W. Mgimwa: Advanced Credit Operations, Dar Es Salaam. 2007
W. Mgimwa: Advanced Treasury Management, Dar Es Salaam. 2009

Wednesday, 1 January 2014

KWA MAISHA YA SASA KUFIKA MIAKA 50 NI NEEMA ZA MUNGU, NA MIAKA 50 YA NDOA NI HAKIKA UKUU WA MUNGU UNADHIHIRIKA KWA FAMILIA HII.

     Wakati binadamu wengi wakililia angalau kufika miaka Hamsini [50] angalau, katika umri wa kawaida. lankini pia fikiri binadamu mwenye umri wa miaka hamsini [50]  anaonekanaje hasa, wengi hujivunia hilo, lakini kwa familia hii ilijivunia tofati kabisa si umri wa kuishi kufikia hapa bali ni kufikisha miaka Hamsini ya Ndoa.
    Ndoa nyingi sana zimekua zikivunjika katika zama hizi na inapotokea unafikisha miaka kumi, ishirini, thelasini, arobaini  na hata Hamsini hakika ni kwa neema za Mungu tu.
   Hivi karibuni Familia ya Anthony Bahati ilishekherekea miaka Hamsini ya ndoa ndugu jamaa na marafiki walijumuika na familia hii kwa kumshukuru Mungu kwa kuilinda na kuisimamia familia hii iliyojaa upendo. wengi tunawaza kufika huko lakini yote ni kwa neema za Mungu.
  

TAZAMA PICHA WAKATI WA SHEREHE HIZO NYUMBANI KWA  FAMILIA YA ANTHONY BAHATI




Tuesday, 31 December 2013

ALOYSIUS PRIMARY AND SECONDARY SCHOOL. SHULE ILIYOLENGA KULETA MAPINDUZI YA ELIMU GEITA NA KANDA YA ZIWA

     Aloysius Primary and Secondary school ni taasisi ya elimu iliyo chini ya kanisa la Roman Catholic Geita. shulee hii ni moja kati ya shule zilizofanya vizuri sana kielim kanda ya ziwa kwa ujumla. katika ziara yake hivi karibuni Mbunge wa Viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata alipata fursa ya kutembelea taasisi hiyo ya elimu na kuwa mgeni rasmi katika Mahafali maalum ya kuwapongeza wanafunzi wa Darasa la saba walifanya vizuri katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi.
     Kabla ya mahafali hayo Mh. Vicky alipata firsa ya kutembelea shule hiyo na kujionea  hali ilivyo ambapo changamoto zifutazo zinaikabili taasisi ya Aloysius. 1. hakuna Maktaba kwa ajili ya wanafunzi kujisomea zaidi.2. vyoo ni vichache ukilinganisha na idadi ya wanafunzi 3. upungufu wa vitabu vya ziada na kiada, 4. hakuna maabara nzuri kwa ajili ya majaribio ya kisayansi 5. hakuna mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaoishi mbali na shule 6. shule haina uzio hivyo kumekuwa na muingiliano baina ya shughuli za kawaida za kijamii na shughuli za kimasomo na hii kupelekea kuwaathiri wanafunzi katika masomo yao.
     katika mahafali hiyo mgeni Rasmi aliahidi kutoa Shilingi Milioni Mbili ili kusaidia kupunguza changamoto zinazowakabili huku akitoa wito kwa jamii na hasa wazazi kusaidia katika kuchangia maendeleo ya kielimu kwa watoto wao na jamii kwa ujumla.

Tazama picha wakati Mh. Vicky Kamata akikagua shule ya msingi na sekondary ya Aloysius.


Mh. Vicky Kamata akikagua madarasa

Ofisi ya Walimu wa shule ya msingi
Vyoo vya wanafunzi ambavyo pia havitoshelezi mahitaji.



     




Thursday, 26 December 2013

WALEMAVU NA WAJANE KUFADHILIWA VYEREHANI ZAID YA 100 NA VICTORIA FOUNDATION KUPUNGUZA UGUMU WA MAISHA

Na Steven Mruma [Geita]

     Walemavu na wajane watanufaika na ufadhili utakaotolewa na Victoria Foundation Kupitia kwa M/kiti wake Mh. Vicky Kamata ambaye ni mbunge wa viti maalum Geita, katika kuwezesha makundi hayo Victoria Foundation Itafadhili Vyerehani Zaidi ya Mia Moja (100+) vya kisasa kutoka Ujerumani na Uholanzi, na si hivyo tu pia Victoria Foundation itafadhili mafunzo ya walemavu hao na jinsi ya kutimia na kufanya matengenezo ya Vyerehani watakavyopatiwa.
    Mafunzo hayo yanataraji kuanza mapema mwakani maeneo ya Nyakato SIDO Mwanza katika Ofisi za SIDO mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya vyerehani vitakavyotolewa kwa walemavu na wajane
    Katika ufadhili huo pia baadhi ya walemavu watapatiwa Tool Box ambazo zitakuwa na vifaa mbalimbali vya ufundi wa Baiskeli na pikipiki ili kuweza kuwasaidia walemavu katika vikundi vyao kujikwamua na ugumu wa maisha,,

    Ufadhili huo pia unalenga kuwapa mitaji wajasiriamali walemavu na wajane ili waweze kuinua bishara zao na kazi zao mbalimbali za kiuchumi ili kuhakikisha wanapunguza ugumu wa maisha.  akizungumza na Viongozi wa Vikundi vya walemavu na wajane waliofika katika hafla fupi ya kutambua na kutafakari jinsi ya kuwapunguzia wajane na walemavu ugumu wa maisha, ambapo mgeni rasmi alikua Mh. Vicky Kamata ambaye aliahidi kupitia Foundation Ya Victoria Foundation Kusaidia na kufadhili miradi hiyo ili kuwawezesha walemavu, watoto yatima, watoto wa mitaani, wajane na walemavu.
   Aidha Mh. Vicky alisema imani yake kubwa mlemavu pekee anayeweza kusimama kama mleamavu ni mlemavu wa akili tu lakini hawa wengine si walemavu na kwamba hilo ni jina tu lakini wanaweza kuyatengeneza maisha yao zaidi ya binadamu wengine waliokamilika viungo vyote.
    Aliongeza pia wanachokosa sana ni kuwezeshana tu na nafasi waliyoipata kutoka Victoria Foundation waitumie kikamilifu na pia ikawe elimu kwa wenzao sehemu mbalimbali kuwa hata walemavu pia wanaweza hasa wakiwezeshwa.


Mh. Vicky Kamata akizungumza na Viongozi wa vikundi mbalimbali vya walemavu na wajane


Picha ya pamoja na viongozi wa vikundi vya walemavu,

Picha ya pamoja na viongozi wa vikundi vya walemavu


 
Mh. Vicky akijiandaa kupiga picha na Viongozi wa vikundi vya wajane.
Picha na Viongozi wa Vikundi vya wajane Geita


Mh. Vicky Akipeana mikono na viongozi wa vikundi vya wajane.


GEITA DOCUMENTARY

Contributors